Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Takriban wiki mbili zimeshapita tangu mfalme wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba aachie albamu yake mpya ‘Only One King’ iliyoundwa na ngoma 16.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

Tangu albamu hiyo kuingia sokoni, mashabiki wengi wamehoji ni sababu gani hasa zilizopelekea bosi huyo wa Kings Music kuipa albamu hiyo jina la ‘Only One King’.

Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na mtangazaji Lil Ommy, Alikiba alifichua kuwa aliamua kuiita albamu hiyo ‘Only One King’ sio kwa sababu ya kujikweza, bali ni katika kuonesha upendo alionao kwa mashabiki zake na kukubali jina la ‘King’, ambalo ametunukiwa na mashabiki zake.

Soma Pia: Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo

"Theme ya album ni Uking, mi sitaki watu wanione kama najikweza sitaki hizo mambo. Ila imekuja hiyo theme kutokana na mfalme huwa ni mmoja tu hana replacement labda afe. Kwa hiyo nikaona niidedicate hiyo theme nanini kama watu wanavyoniita King Kiba niidedicate tu kwa mafans wangu basi," alizungumza Alikiba.

Aidha, kwenye mahojiano hayo, Alikiba aliongeza kuwa zamani alikuwa anatoa ngoma chache kwa mwaka kwa sababu za kibiashara, na pia alikuwa anatumia muda mwingi studio ili aweze kutengeneza muziki utakaoishi muda mrefu.

"Branding yangu mi muziki nimeibrand kwamba ni lazima muziki wangu uweze kurudisha pesa kwanza alafu nitoe mwingine na nilikuwa najitahidi kutoa muziki ambao utakaa kwa muda mrefu nashukuru Mungu nimeweza kufanya hivyo mara nyingi," alizungumza Alikiba.

Leave your comment