Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo

[Picha : MIllard Ayo]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Siku chache zilizopita, mwanamuziki Patoranking kutokea nchini Nigeria alionekana huko visiwani Zanzibar akiwa na ukaribu na wasanii watanzania kama Nandy, Jux na Alikiba ambaye wengi walishuku kuwa amekuja kufanya nae video.

Soma Pia: Jux, Nandy Waashiria Ujio wa Kolabo na Patoranking

Patoranking amejijengea utamaduni wa kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti wa Tanzania, na makala hii inaangazia ngoma tano ambazo ameshashirikiana na wasanii watanzania.

  1. Bajaj - Navy Kenzo

Ngoma hii ilitoka Februari mwaka 2017 na inapatikana kwenye albamu ya Navy Kenzo ya kuitwa ‘Above In A Minute’. ‘Bajaj’ ni ngoma ambayo Nahreel aliweza kuiandaa yeye mwenyewe. Ndani ya ngoma hii Navy Kenzo na Patoranking wanaimba kwa ustadi mkubwa huku wakiwahasa wanaume wote kuwa na tabia ya kuwaheshimu wanawake.

https://www.youtube.com/watch?v=jZJe2f8P9wo

  1. Tetema Remix - Rayvanny

Baada ya ‘Tetema’  kufanya vizuri, Patoranking hakuona hatari kuingia kwenye remix ya ngoma hiyo ambayo iliachiwa mwezi Agosti mwaka 2019. Mpaka sasa, remix hio imeshatazamwa mara milioni 6.7 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=yOoqfaetRdc

  1. Namna Gani - Walid

Mwaka 2018 mwanamuziki Walid alipata nafasi ya kumshirikisha Patoranking kwenye ngoma ‘Namna Gani’. Ngoma hii ambayo kila unapoisikia unaweza kudhani ni mpya ina mahadhi ya densi. Clarence Peters kutokea nchini Nigeria alihusika katika kuandaa video yake.

https://www.youtube.com/watch?v=0YurpnkWnCo

  1. Love You Die - Diamond Platnumz

Kama kuna ngoma ambayo iliweza kukita na kufanya vizuri sana kwenye mitaa mbalimbali nchini Tanzania basi ni ‘Love You Die’ kutoka kwa Patoranking akimshirikisha Diamond Platnumz. Ngoma ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni hamsini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ZjN4agWqTdc

  1. Bwana Mdogo - Alikiba

Ngoma namba tisa kwenye albamu yake ya ‘Only One King’. Alikiba aliweza kumshirikisha Patoranking ambaye anasikika zaidi kwenye aya ya pili ya ngoma hii ambayo imeandaliwa na Yogo Beats. Kufikia sasa, wimbo huu umeshatazamwa mara laki tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=bmPIjtnY3iA

 

Leave your comment