Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni siku njema sana kwa mashabiki wa muziki nchini Tanzania kwani hatimaye mwanamuziki Alikiba ameachia albamu yake ‘Only One King’ ambayo imeshonwa na ngoma 16.

Soma Pia: Albamu 3 Zitakazosisimua Tasnia ya Muziki Tanzania

Ifuatayo ngi uchambuzi wa ngoma zilizo kwenye albamu hio:

Oya Oya

Kwenye ngoma hii ambayo inakata utepe wa albamu, Alikiba anaimba kwa bashasha zote jinsi anavyomhusudu mpenzi wake ambaye amedhamiria kumuoa.

https://www.youtube.com/watch?v=HiX-aYj2yas

Amour

‘Amour’ ni neno la kifaransa lenye maana ya upendo. Tofauti na ngoma ya ‘Oya Oya’, ndani ya ‘Amour’, Kiba anaimba kwa staha na utaratibu kuonesha jinsi mapenzi yalivyomkamata na kumshika kisawasawa kiasi cha kuwa tayari hata kufunga pingu za maisha na mchumba wake.

https://www.youtube.com/watch?v=hl5v5dQvvS8

Tamba ft Tommy Flavor, K2ga & Abdu Kiba

Kwa mara nyingine tena Alikiba anashirikiana na vijana wake wa Kings Music. Kwenye ‘Tamba’, Kiba anampa pongezi mke wake kwa kumzalia mtoto wa kufanana nae. Ngoma hii bila shaka itafaa mno kwenye sherehe za ‘Baby Shower’ ambazo watoto wachanga hutambulishwa rasmi kwa jamii.

https://www.youtube.com/watch?v=RPWpPPeB-JI

Sitaki Tena

Hii ni moja kati ya ngoma nyepesi zenye mashairi ya kukaririka kwa haraka. Alikiba anaimba kwa hisia kuwa hataki tena mahusiano na mpenzi wake wa zamani hata baada ya kuombwa msamaha.

https://www.youtube.com/watch?v=Ra52ztFZmaw

Washa ft Nyashinski

Kwenye ngoma hii, Alikiba na Nyashinski wanatupa mawe gizani kwa wale watu ambao wanajaribu kukwamisha mahusiano ya watu wengine. Kilichonogesha zaidi ngoma hii ni mdundo mkali kutoka kwa Yogo Beats.

https://www.youtube.com/watch?v=_wbK-_YWYs0

Bwana Mdogo ft Patoranking

Kama unatafuta ngoma ambayo utaicheza ukiwa club na marafiki basi bila shaka ‘Bwana Mdogo’ imekamilisha lengo. Kwenye wimbo huu, Alikiba na Patoranking wanaonesha furaha walizonazo baada ya kupata wenza wa maisha yao pamoja na raha inayokuja ukiwa kwenye mahusiano yenye afya.

https://www.youtube.com/watch?v=bmPIjtnY3iA

Habibty ft Khaligraph Jones

Katika ‘Habibty’, Alikiba anamuomba mpenzi wake apunguze wivu na anatumia sauti yake yenye ushawishi mkubwa kumhakikishia mwenza wake kuwa atakuwa mwaminifu. Kwenye aya ya pili, Khaligraph anaingia na kukoleza zaidi ujumbe huo wa Alikiba.

https://www.youtube.com/watch?v=R1ODhgt2JqY

Gimme Dat

Huu ni wimbo ambao Alikiba anagusa hisia za watu wanaopenda kujiachia na kwenda viwanja kipindi cha mwisho wa wiki. Kwenye ngoma hii, Kiba anatawaliwa na utulivu kwenye sauti yake.

https://www.youtube.com/watch?v=EliMI2i78DU

Niteke  ft Blaq Diamond

Alikiba anamshirikisha Blaq Diamond kutokea Afrika kusini kwenye ngoma hii ambayo ndani yake anaomba kupewa zaidi mapenzi motomoto na mwandani wake.

https://www.youtube.com/watch?v=CPfxfbzZRXY

Let me ft Sauti Sol

Wimbo huu ni kama barua ya mapenzi ambayo Alikiba anashirikiana na Sauti Sol kuiandika. Kwenye ngoma hii, Kiba anatoa shukrani kwa kumpata mpenzi wa ndoto zake.

https://www.youtube.com/watch?v=gkReel6mzq0

Utu

Alikiba anaamua kukiri furaha na raha anayoipata kutoka kwa mpenzi wake kupitia ngoma hii ya ‘Utu’.Pia anaonesha kufurahia mahusiano aliyonayo kwa kuonesh kuwa yuko radhi hata kufa kwa ajili ya mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=7LWCBhMH798

Happy ft Sarkodie

Hii ni ngoma inayofunga pazia la albamu. Alikiba anaimba kwa hisia sana kuhusu furaha anayoipata kwenye mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=CjljpOF9LIU

Nyimbo zingine zilizo kwenye albamu ni kama vile ‘Jealous’, ‘Salute’, ‘Infidele’ na ‘Ndombolo’ambazo ziliachiwa kabla ya uzinduzi rasmi ya alabamu hio.

https://www.youtube.com/watch?v=LQyCY1t--GU

Leave your comment