Albamu 3 Zitakazosisimua Tasnia ya Muziki Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ushindani mkubwa uliopo baina ya wasanii wakubwa nchini Tanzania umezalisha uwepo wa albamu ambazo zitasisimua, na huenda zikapandisha hadhi ya tasnia ya muziki ya Tanzania.

Wasanii wakubwa watatu kutoka bongo wakiwemo; Alikiba, Harmonize na Diamond Platnumz mwaka huu walitangaza kuwa wataachia albamu zao. Matangazo hayo yaliongeza joto kwenye muziki kwani hii ni mojawapo ya fursa ya wasanii hao kuonyesha nani bingwa na fundi wa muziki zaidi ya mwingine.

Soma Pia: Wasanii wa Afrika Mashariki, Magharibi Watawala Albamu Mpya ya Alikiba ‘Only One King’

Ushindani baina ya albamu hizi tatu ni mkubwa kwa kiasi kwamba Diamond na Harmonize walisafiri kuenda ng'ambo kusudi kupata ufundi wa watayarishaji wa miziki kutoka nchi za kigeni.

Mwanamuziki wa kwanza kudondosha albamu yake ni Alikiba ambaye ameachia rasmi albamu yake tarehe saba mwezi huu. Albamu hiyo ambayo ni ya tatu kutoka kwa Alikiba, ina jumla ya nyimbo kumi na sita na imewahusisha wasanii kutoka nchi tofauti za bara la Afrika.

Aliyesimamia utengenezaji wa albamu hiyo ni mtayarishaji wa muziki Yogo Beats kutoka Tanzania.

Kwa upande mwingine, msanii Harmonize ambaye pia ni bosi wa Konde Music Worldwide tayari ashafichua kuwa albamu yake itakayofuatia imepewa jina la ‘High School’.Japo habari zipo finyu kuhusiana na albamu hiyo, alichokiweka wazi msanii huyo ni kuwa kwa sasa anashughulikia utayarishaji wake.

Soma Pia: Enock Bella Aeleza Sabau ya Wimbo Wake Na Mbosso Kutolewa Kwenye ‘Definition of Love’ Album

Albamu nyingine ambayo ipo kinywani mwa wengi ni kutoka kwa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz. Simba anatarajiwa kunguruma mwaka huu na kudhibitisha kuwa yeye ndiye mfalme kwenye pori la muziki. Diamond kwa siku za hivi karibuni amekutana na wadau wakubwa sana kwenye tasnia ya muziki ya Marekani kwa shughuli nzima ya kufanikisha albamu yake.

Leave your comment