Wasanii wa Afrika Mashariki, Magharibi Watawala Albamu Mpya ya Alikiba ‘Only One King’
6 October 2021
[Picha: Alikiba Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Orodha ya nyimbo zilizoko kwenye albamu ya Alikiba hatimaye imetoka. Albamu hiyo ambayo iko na jumla ya nyimbo kumi na sita inatarajiwa kuachiwa rasmi tarehe saba mwezi Octoba.
Alikiba hapo awali wakati wa utambulisho wa albamu hiyo aliwaahidi mashabiki kolabo chungu nzima . Albamu hiyo ambayo ni ya tatu kutoka kwa msanii huyo, imetawaliwa na kolabo zinazowahusisha wasanii kutoka mataifa tofauti barani Afrika.
Soma Pia: Alikiba Amkaribisha Patoranking Tanzania
Wengi wa wasanii walioshirikishwa kwenye albamu hio aidha wanatoka Afrika Mashariki au Afrika Magharibi. Kwa jumla, albamu hiyo iko na kolabo tisa.
Kolabo ya kwanza ni kwenye ngoma iitwayo 'Tamba'. Alikiba ameshirikiana na msanii Tommy Flavour ambaye amesainiwa katika lebo yake ya Kings Music. Kolabo ya pili ambayo imeorodheshwa namba nne kwenye albamu hiyo ni wimbo wa 'Jealous' ambao Alikiba alimshirikisha msanii Mayorkun kutoka Nigeria.
Alikiba vilevile amemshirikisha msanii Rude Boy kutoka Nigeria kwenye wimbo wa 'Salute' ambao tayari ushatoka.
Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kutofanya Swahili Amapiano Licha ya Umaarufu wa Mtindo Huo
Msanii mwingine wa kutajika kutoka Nigeria ambaye pia alipata fursa ya kufanya kazi na Alikiba ni Patoranking kwenye ngoma iliyopewa jina la 'Bwana Mdogo' na Sarkodie kwenye ‘Happy’.
Wasanii kutoka nchini Kenya pia hawajaachwa nyuma katika albamu hiyo iliyopewa jina la Only One King. Nyashinski, Sauti Sol na Khaligraph Jones walipata nafasi ya kutia ustadi wao katika nyimbo tofauti.
Leave your comment