Alikiba Amkaribisha Patoranking Tanzania

[Picha: rickmediatz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria Patoranking kwa sasa yupo Tanzania ambako alikaribishwa na staa wa muziki Alikiba.

Japo Patoranking hakutangaza ziara yake ya Tanzania, picha na video zimeibuka mtandaoni zikimwonyesha akiwa pamoja na Alikiba. Sababu kuu ya Patoranking kutua Tanzania bado haijulikani ila wengi wanaamini kuwa huwenda ikahusiana na albamu ya Alikiba ambayo inatarajiwa kutoka tarehe saba mwezi huu.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kutofanya Swahili Amapiano Licha ya Umaarufu wa Mtindo Huo

Patoranking ni mwanamuziki mwenye heshima kubwa si Afrika tu bali duniani nzima. Amewahi kufanya kazi na wanamuziki wa Tanzania ikiwemo Diamond Platnumz kwenye wimbo wa 'Love You Die' ambayo iliteka anga za muziki na kuvuma sana.

Kufikia sasa, takriban miaka minne baada ya kuachiwa, ngoma hiyo imetazamwa takriban mara milioni hamsini na tatu.

Kutua kwa Patoranking Tanzania kunatokea muda mfupi baada ya Alikiba kutambulisha rasmi albamu yake ambayo ameipa jina la Only One King'. Alikiba wakati wa utambulisho huo alifichua kuwa kwenye albamu hiyo amefanya kazi na wanamuziki wengi sana kutoka pande tofauti za bara la Afrika.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Jina na Siku Atakayoachia Albamu Yake Mpya

Kwa mujibu wa Alikiba, mashabiki wake walikua wakilalamika kuwa hafanyi kolabo za kutosha na hivyo basi akaamua kwa upendo wa mashabiki kufanya kolabo nyingi.

"In general, muziki wangu sijakuwa nikifanya collaboration, lakini nimeamua kufanya safari hii kwa kuwaonyesha kwamba nimeskia kelele zao na kwa mapenzi na kuheshimisha juu yake nikaamua acha nifanye tu albamu," Alikiba alisema.

Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kwa hamu sana siku kuu ya kuachiwa kwa albamu hiyo.

Leave your comment