Alikiba Atangaza Jina na Siku Atakayoachia Albamu Yake Mpya

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki wa bongo Alikiba hatimaye ametambulisha rasmi jina la albamu yake iliyosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wake.

Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii na pia kikao na wanahabari alifichua kuwaalbamu hio amlipa jina la "Only One King" na itatoka tarehe saba mwezi ujao.

Soma Pia: Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings Music alitaja albamu hiyo kama zawadi kwa mashabiki wake huku akiongezea kuwa watarajie kuburudishwa na muziki mzuri.

"Ningependa kutambulisha kwenu rasmi jina na cover art ya album yangu mpya ‘Only One King’ hii ni zawadi yangu kwenu mashabiki na wapenda muziki mzuri. itatoka rasmi tarehe 07.10.2021," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Katika kikao na wanahabari, Alikiba alisema kuwa sababu kuu iliyomsukuma kutoa albamu ilikuwa malalamiko kutoka kwa mashabiki wake ambao walidai kuwa hafanyi kolabo kwa kiwango wanachokitaka.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu Kuu Iliyochelewesha Albamu Yake

Aliongeza kuwa albamu hiyo iko na kolabo kadhaa. Mwanamuziki huyo alidai kuwa albamu ndio njia mwafaka ya msanii kujitambulisha kwa mashabiki.

Alifafanua kuwa albamu inampea shabiki ladha tofauti ya nyimbo na hivyo basi, shabiki ataweza kubaini iwapo msanii anabahatisha au ako na talanta.

"In general muziki wangu sijakuwa nikifanya collaboration, lakini nimeamua kufanya safari hii kwa kuwaonyesha kwamba nimeskia kelele zao na kwa mapenzi na kuheshimisha juu yake nikaamua acha nifanye tu albamu," Alikiba alisema.

Leave your comment