Alikiba Afichua Sababu ya Kutofanya Swahili Amapiano Licha ya Umaarufu wa Mtindo Huo

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mflame wa muziki wa bongo Alikiba amefichua sababu ya yeye kutofanya mtindo wa Swahili mapiano licha ya mtindo huo kupata umaarufu sana kwa siku za hivi karibuni.

Swahili Amapiano ulikuja na ukavuma sana kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania huku wasanii wengi wakubwa wakitoa nyimbo kwa mtindo huo. Baadhi ya wasanii wenye hadhi ya juu ambao walitoa ngoma za Swahili Amapiano ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Marioo na wengine wengi.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Jina na Siku Atakayoachia Albamu Yake Mpya

Alikiba hata hivyo amekwamilia mtindo wake wa bongo na mawimbi ya Swahili Amapiano hayajamtetemesha hata kidogo.

Akizungumza na wanahabari wakati anatambulisha rasmi albamu yake iitwayo ‘Only One King’, Alikiba alifunguka kuhusu uamuzi wake wa kutofanya Swahili Amapiano.

Msanii huyo alisema kuwa amewaachia wanamuziki wengine wafanye mtindo huo huku yeye akifanya mtindo wake. Alikiba hata hivyo alisifia Swahili Amapiano kwa kusema kuwa ni muziki mzuri ambao umepata mashabiki wengi.

Soma Pia: Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

"Ni muziki ambao unafanya vizuri, na watu wamekuwa wanaupenda na umepata mafans wengi sana. Na huwezi mkataza mtu kupenda muziki kwa sababu ni kosa la jinahi," Alikiba alitoa kauli yake kuhusu Swahili Amapiano.

Alikiba hata hivyo alifichua kuwa kwenya albamu yake inayokuja amefanya kazi na wasanii kutoka Afrika Kusini ambako mtindo wa amapiano unatoka. Ila aliongezea kwa haraka kuwa sio kila muziki unaotoka Afrika Kusini ni wa Amapiano.

Leave your comment