Enock Bella Aeleza Sabau ya Wimbo Wake Na Mbosso Kutolewa Kwenye ‘Definition of Love’ Album

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya kuwepo tetesi kuwa Mbosso alifuta wimbo aliofanya na Enock Bella, na uliotakiwa kuwepo kwenye albamu ya "Definition Of Love" iliyoachiwa mwezi Machi mwaka huu, hatimaye Enock Bella amejitokeza kuzungumzia tetesi hizo.

Enock Bella ameeleza kuwa ni kweli yeye na Mbosso walifanya ngoma ya pamoja, lakini uongozi wa WCB walimshauri Mbosso kuwa ngoma yake na Enock Bella inafaa kuachiwa kama wimbo wa kawaida tu, ili ufanye vizuri zaidi.

Soma Pia: Cheed Aeleza Chanzo Cha Ukimya Wake Tangu Ajiunge na Konde Gang 

 "Mbosso aliniletea wazo akaniuliza unaonaje? Uongozi ulikuwa umesema hii ngoma isiwepo kwenye albamu lakini hii ngoma itoke kama single, ikiwa kwenye albam kidogo itakuwa haiwezi kukupa nguvu hatuwezi kupata kile ambacho sisi tunakihitaji lakini ikiwepo kama single tutaweza kupata nguvu sana hata mimi pia nikawa nime-appreciate hicho kitu," alizungumza Bella.

Soma Pia: Tommy Flavour Azungumzia Uwezekano wa Collabo na Zuchu

 Pia Enock Bella aliendelea kuzungumza kuwa yeye hana tatizo kabisa na Mbosso kama ambavyo wengi wamekuwa wakisema huko mtandaoni.

"Tunakuwa karibu (na Mbosso) lakini hatuwi close sana tutakuwa vitu vingine hatuwezi kuvifanya tutakuwa tunaviharibu lazima na yeye kuna vitu vingine avifanye vitu vingine mi nifanye binafsi," alizungumza Enock Bella.

Enock Bella na Mbosso wote wawili walikuwa kwenye kundi la Yamoto Band wakiwa pamoja na Beka Flavour na Aslay japo kundi hilo lilivunjika mwaka 2017.

Leave your comment