Cheed Aeleza Chanzo Cha Ukimya Wake Tangu Ajiunge na Konde Gang

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki iliyopita, mwamuziki Cheed aliachia ngoma yake ya kwanza ‘Wandia’ tangu ajiunge na lebo ya Konde Gang zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Wengi wamekuwa wakiuliza ni kwa nini Cheed amekuwa kimya sana, hasa baada ya kutoka Kings Music na kujiunga na Konde Gang.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Akizungumza hivi karibuni, Cheed alisema ukimya wake ni kutokana na kuandaa albamu yake ya kwanza chini ya lebo hiyo, na kwa sasa ana nyimbo nyingi sana ambazo anatarajia kuziachia.

"Nilikuwa nimekaa kimya ili kuandaa muziki mzuri na sasa nina stock ya kutosha na niko tayari hata kutoa albamu so mashabiki zangu wamenivumilia kwa muda mrefu sana lakini sasa ndio wakati wa back to back," alizungumza msanii huyo.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny, Harmonize, Zuchu na Mbosso Waongoza Wasanii Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Septemba

Cheed sio msanii pekee kutokea Konde Gang ambaye ametangaza kutoa albamu wengineo ni pamoja na bosi wa lebo hiyo Harmonize, Killy na Ibraah ambaye sasa anatamba na ‘Jipinde’.

 Cheed pia alizungumza kwamba anajivunia kuwa chini ya Konde Gang na hata mara moja hajawahi kuwa na majuto kuwa chini ya lebo hiyo.

"Mimi hapa kiukweli tangu nimekuwa signed chini ya Konde Gang nimekuwa nikijivunia sana sijawahi kufikiria hiyo kujutia wala kitu chochote kwa sababu kila kitu kiko on set yaani kimekaa vizuri," alizungumza Cheed.

Leave your comment