Diamond, Rayvanny, Harmonize, Zuchu na Mbosso Waongoza Wasanii Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Septemba

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwezi Septemba 2021 ulikuwa ni mwezi wenye maana sana kwenye tasnia ya muziki hapa Tanzania kwani wasanii wengi waliachia ngoma mpya. Kulingana na orodha iliyoachiwa na YouTube, wafuatao ni wasanii watano ambao wametazamwa zaidi kwenye mtandao huo mwezi Septemba mwaka huu:

Soma Pia: Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’, Rayvanny ‘Wanaweweseka’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania

Diamond Platnumz

Bosi huyu wa lebo ya WCB kwa mwezi Septemba ametazamwa mara Milioni 33.4 kwenye mtandao huo. Diamond na ndiye msanii anayeongoza kutazamwa zaidi Tanzania kwenye YouTube. Video ya ‘Naanzaje’ imeweza kufanya vizuri na kupokelewa na mashabiki kwa mikono miwili kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 8.4.

Rayvanny

Rayvanny ni msanii wa pili kutazamwa zaidi YouTube kwa mwezi Septemba. Msanii huyo ametazamwa mara milioni 23.4 kwenye mtandao huo. Video yake ya ‘Wanaweweseka’ iliyotoka wiki tatu nyuma imeshatazamwa mara milioni 3.4 kwenye mtandao huo.

Harmonize

Mwezi Septemba, Harmonize ametazamwa mara Milioni 16.7 kwenye mtandao huo, huku video yake ya ‘Teacher’ ikiwa imeshatazamwa mara milioni 4.8.

Mbosso

Mbosso anashika nafasi ya nne kwa kutazamwa zaidi YouTube mwezi Septemba. Kazi zake zote zimetazamwa mara Milioni 15.7 kwenye mtandao wa YouTube. Kikubwa kuhusu Mbosso ni kuwa mwezi Septemba hakuachia video yoyote na bado ameendelea kufanya vizuri kwenye mtandao huo.

Soma Pia:  Diamond Platnumz Atuma Ujumbe kwa Mashabiki Kupitia Wimbo wa 'Kamwambie'

Zuchu

Zuchu anashikilia nambari tano kwenye orodha hii kwani ametazamwa milioni 13.4. Ngoma ya mwisho kutoka kwa Zuchu ilikuwa ni ‘Yalaaaa’ ambayo iliingia sokoni mwezi Agosti.

Leave your comment