Diamond Platnumz Atuma Ujumbe kwa Mashabiki Kupitia Wimbo wa 'Kamwambie'

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota Diamond Platnumz amesifiwa kwa mafanikio yake makubwa kwenye tasnia ya muziki. Simba, kama anavyojulikana kiusanii, ameorodheshwa miongoni mwa wanamuziki wenye kipato kikubwa sana katika bara la Afrika.

Safari ya Diamond kwenye muziki, hata hivyo, ilianza mbali wakati akiwa bado mwanamuziki mchanga. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliwarudisha mashabiki wake nyuma na kuwakumbusha wimbo wake wa 'Kamwambie' alioutoa wakati akiwa mchanga kimuziki.

Soma Pia: Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’, Rayvanny ‘Wanaweweseka’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania

Diamond kwenye chapisho lake aliwashauri mashabiki wake kutokata tamaa na kumtumia yeye kama ushuhuda kuwa bidii na ubunifu huleta matunda.

Alisema kuwa wimbo wake wa 'Kamwambie' uwe kumbusho kuwa licha ya shida ambazo mtu anapitia maishani, kuwa ipo siku zitaisha.

Msanii huyo aliongeza kuwa maombi, heshima na ubunifu ni vitu vya maana sana kwa mtu anayetaka kufaulu maishani.

"Kila Unapojihisi kukata tamaa play hii nyimbo, ikukumbushe kuwa tabu unazopitia leo kuna siku zitaisha.. Sali sana, Ongeza bidii na Ubunifu kwenye ulifanyalo, Muheshim kila mtu na Mwenyez Mungu atakufungulia," ujumbe wa Diamond Platnumz mtandaoni ulisomeka.

Soma Pia: Babu Tale Azungumzia Diamond Kulinganishwa na Wasanii wa Nigeria

Kando na kuwa mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa duniani, Diamond pia anamiliki Wasafi FM, Wasafi TV na lebo ya WCB.

Kwa sasa, Diamond yupo kweye harakati ya kufanikisha ziara yake ya muziki nchini Marekani. Diamond pia anatarajiwa kuachia albamu yake hivi karibuni ambayo amewashirikisha wadau mbali mbali kutoka nchi za ng'ambo.

Leave your comment