Babu Tale Azungumzia Diamond Kulinganishwa na Wasanii wa Nigeria

[Picha: All Star]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz ametoa ushauri mzito kwa mashabiki wanaomfananisha msanii wake na wasanii wakubwa wa Nigeria kama Burna Boy na Wizkid.

Babu Tale ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini mashariki, amezungumza kuwa Diamond ni msanii wa ajabu mwenye kipaji kikubwa na anayetumia lugha ya Kiswahili, lakini bado anashindanishwa na wasanii wa Nigeria ambao wanatumia lugha ya kiingereza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo 'Samia Suluhu'

"Kwa msanii anayeongea kiswahili anayeimba kiswahili na anaenda kufananishwa na wasanii wanaoimba kizungu. Diamond sio msanii wa kawaida," alizungumza Babu Tale.

Kauli hii ya Babu Tale inathibitishwa dhahiri shahiri kwenye tuzo za Afrimma za mwaka 2021 ambapo msanii Diamond Platnumz amewekwa kuwania tuzo kwenye kipengele kimoja cha msanii bora Afrika kwa mwaka 2021, kipengele ambacho ameshindanishwa na mshindi wa tuzo ya BET Davido, Wizkid pamoja na mshindi wa tuzo ya Grammy kwa mwaka 2021 Burna Boy.

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy Alikiba, Darassa, Harmonize na Rayvanny Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMA 2021

Aidha, Babu Tale pia alizungumzia kuhusu albamu ya Diamond Platnumz ambayo iko mbioni kuachiwa kwa kusema kuwa watanzania wataelewa ukubwa wa Diamond Platnumz wakishasikiliza albamu yake.

"Najua albamu ya Diamond ikoje na kwa kuwa najua albamu ya Diamond ikoje wasubirie waje waone albamu ya Diamond ikoje," aliongea Babu Tale kwa bashasha kubwa.

Leave your comment