Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo 'Samia Suluhu'

[Picha: Afrika Lyrics]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutokea Tanzania Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya uitwao 'Samia Suluhu'. Wimbo huu unamsifia rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Diamond anammiminia sifa kiongozi huyo kwa maendeleo ambayo ameileta Tanzania tangu kuchukua usukani kama rais.

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy Alikiba, Darassa, Harmonize na Rayvanny Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMA 2021

"Ameimarisha urafiki, kimataifa. Wawekezaji sa nchini, kwetu wanafika. Demokrasia siasa ya kuridhisha. Biashara oona zinauzika. Aise nampenda Samia. Uonevu hataki Samia. Mikopo elimu kaweka safi, Samia. Mashule kwa zahanati, Samia. Kapinga zile kodi zote zisohalali. Vina uhuru sasa, vyombo vya habari. Zote kesi za uonevu, kafutilia mbali. Kapunguza faini za boda boda. Sasa mambo shwari,"Diamond anaimba kwenye ngoma hiyo.

Ngoma hiyo imetayarishwa chini ya usimamizi wa lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond.

Kufikia sasa, ngoma hiyo imetolewa kwa mfumo wa audio tu. Diamond hajadhibitisha siku rasmi atakayoachia video ya wimbo huu.

Soma Pia: Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo

Kilichofurahisha wengi ni jinsi Diamond alitumia mistari kutoka kwa nyimbo zake zingine katika ngoma hii. Mchanganyo huo uliongeza ladha wa wimbo na pia kudhihirisha ustadi wa Diamond katika muziki.

'Samia Suluhu' imepokelewa vyema na mashabiki na imetazamwa takriban mara laki nne ndani ya masaa arobaini na nane.

Si jambo geni kuona msanii akitoa wimbo wa kusifia kiongozi nchini Tanzania. Hapo awali msanii maarufu Zuchu kutokea lebo ya WCB pia alitoa wimbo wa kumsifia rais Samia Suluhu. Hayati rais John Maghufuli Pombe pia ni kiongozi ambaye alimiminiwa sifa sana na wasanii.

https://www.youtube.com/watch?v=yONuS8TB13M

Leave your comment