Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’, Rayvanny ‘Wanaweweseka’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nchini Tanzania mambo yameendelea kuwa motomoto kwenye kiwanda cha muziki hasa kwenye mtandao wa YouTube ambapo baadhi ya ngoma mpya zilizoachiwa zinaendalea kufanya vizuri. Kwenye nakala hii, tunaangazia ngoma tano ambazo zimefanya vizuri sana kwenye upande wa YouTube:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya Wimbo wa 'Yuda'

Sina Neno - Jux

Jux ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya ngoma yake ya ‘Sina Neno’ kushika namba moja wiki hii upande wa YouTube. Beat kali kutoka kwa Bob Manecky pamoja na video yenye viwango kutoka kwa Hanscana vimeheshimisha ngoma hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa zaid ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=cDxZrTIcKLk

Naanzaje - Diamond Platnumz

Kwa wiki ya tatu mfululizo, Diamond Platnumz ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Naanzaje’ iliyotayarishwa na Lizer Classic. Kufikia sasa, video ya ngoma hii imeshatazamwa mara Milioni 7.9 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Wanaweweseka - Rayvanny

Tangu Rayvanny aachie ‘Wanaweweseka’ Septemba 10 mwaka huu, ngoma hiyo imeendelea kufanya vizuri kutokana na mashahiri yake mazuri. Ngoma hii mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube imeshatazamwa mara Milioni 3.3.

https://www.youtube.com/watch?v=M6WisT8ocUE

Size Yao - Darassa ft Dogo Janja

Wiki hii, Darassa aliamua kutoa video ya ‘Size Yao’ aliyomshirikisha Dogo Janja. Kwenye ngoma hii, wanafurahi maisha waliyonayo kwa sasa kwani wametokea kwenye hali ya duni. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki tatu themanini na nne elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=f6v0V8ZAeqo

 Jah Jah - Tommy Flavour ft Alikiba

Tommy Flavor ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jah Jah’ aliyomshirikisha Alikiba. na kwa mujibu wa Tommy Flavor alidokeza kuwa huo ni wimbo wa kwanza kutoka kwenye album yake ya "Heir To The Throne" ambayo ipo mbioni kuingia sokoni.

https://www.youtube.com/watch?v=IM0Rs05yiSw

Leave your comment