Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya Wimbo wa 'Yuda'
1 October 2021
[Picha: Nandy Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Malkia wa muziki wa bongo Nandy ameachia video ya wimbo wake wa 'Yuda'.
Ngoma hii inazungumzia mapenzi yaliyonoga baina ya wachumba wawili. Nandy anaimba na kumsifia mpenzi wake kwa upendo ambao anapata kwenye mahusiano yao.
Soma Pia: Zuchu Amsifia Nandy, Adokeza Kuwa Hana Tatizo Kufanya Kolabo Naye
"Nimemyosha wangu Yuda. Vyake vitamu najipakulia. Kungwi nimefundo. Wake ma ex ndo wanaumia. Walisema limevunda. Sasa jikoni ndo linanukia. Ye ndo wangu kiti. Tena hachoki nikimkalia. Na tena siku hizi nanenepa nanawiri. Yamenoga mapenzi na yameshamiri. Anipa vidogo na vikubwa tamu sio shubiri. Nyumbani kumenoga huniponza mwili," Nandy anaimba katika wimbo huo wa 'Yuda'.
Mdundo wa ngoma hii imetengenezwa na mtayarishaji wa muziki Kimambo Beats. Kimambo Beats amefanya kazi na Nandy kwa muda mrefu na mara kwa mara wanaposhirikiana katika wimbo, huwa inaishia kuvuma.
Video kwa upande mwingine imeelekezwa na Ivan. Video ya wimbo huu inaendana na ujumbe uliopo kwenye wimbo. Kwa asilimia kubwa ya video, Nandy anaonekana akifurahia kuwa na mpenzi wake.
Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya
'Yuda' imepokelewa vyema na mashabiki na tayari ishapata maelfu ya watazamaji ndani ya muda mfupi.
'Yuda' ni miongoni mwa nyimbo nne ambazo zinapatikana kwenye EP ya Nandy iliyopewa jina la 'Taste'. Nyimbo nyingine zilizopo kwenye EP hiyo ni pamoja na; 'Nimekuzoea', 'New Couple' na 'Yote Sawa'.
'Yuda' ndio video ya pili ambayo Nandy anaachia baada ya kutoa video ya 'Nimekuzoea'.
Leave your comment