Baba Levo Azungumzia Tetesi za Hanstone Kuondoka WCB

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na rapa maarufu nchini Tanzania Baba Levo kwa mara ya kwanza amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tetesi za hivi karibuni kuhusu mwanamuziki Hanstone kujiondoa WCB.

Kwa muda mrefu sasa, Hanstone alikuwa na ukaribu mkubwa na lebo ya WCB kiasi cha watu kusema kuwa tayari ameshajiunga na lebo hiyo kubwa Afrika Mashariki lakini.

Soma Pia: Harmonize Aachia Kionjo cha Wimbo Wake Mpya ‘Single’

Minong'ono hiyo ilizimika siku chache nyuma baada ya Hanstone kuachia EP yake ya kuitwa "Amaizing" kwenye mitandao mbalimbali ya kutiririsha muziki.

Baba Levo ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Mgahawa kwenye Wasafi FM akiongea na waandishi wa habari, amethibitisha kuwa tetesi hizo za Hanstone kuondoka WCB ni za ukweli.

Soma Pia: Producer Bob Maneke Afichua Mchango wa Rayvanny Kwenye Wimbo wa Jux 'Sina Neno'

"Nilikaa mimi, yeye (Hanstone) na Diamond. Diamond akamwambia Hanstone nataka nikutoe mwezi wa tano. Naomba uniletee nyimbo tano ambazo zimekamilika. Nyimbo tano zilizokamilika hana (Hanstone). Nilitaka kumpiga vibao. Nikamwambia kumbe wewe dogo wewe haujitambui," alizungumza Baba Levo.

Baba Levo alieleza zaidi kuwa baada ya kikao hicho ndipo Hanstone alianza kurekodi nyimbo tofauti tofauti na Diamond Platnumz alimwambia Baba Levo kuwa atamtambulisha rasmi msanii huyo mara tu atakaporudi kwenye ziara yake anayofanya nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Baba Levo, mambo yalienda mrama baada ya msanii huyo kuachia EP hiyo bila idhini ya WCB.

"Diamond akaniambia nikitoka Marekani namsurprise huyu dogo, nikitoka Marekani namuachia. Yuko Marekani (Diamond Platnumz) dogo kachapa EP," aliongeza Baba Levo.

Hanstone ni mojawapo ya wasanii wachanga wenye karama kubwa ya uandishi wa nyimbo kwani ameshiriki kuandika nyimbo ya Maua Sama ‘Iokote’ na ‘Chibonge’ ya Abbah Process.

Leave your comment