Producer Bob Maneke Afichua Mchango wa Rayvanny Kwenye Wimbo wa Jux 'Sina Neno'

[Picha: Jux Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wimbo wa 'Sina Neno' kutoka kwa mwanamuziki Jux ulizua gumzo sana mtandaoni kutokana na maudhui yake yaliyohusishwa na mpenzi wa zamani wa msanii huyo Vannessa Mdee.

Ngoma hiyo ilitoka muda mfupi baada ya habari kuibuka kuwa Vannessa Mdee, ambaye pia alikuwa mwanamuziki kabla ya kustaafu, alikua mja mzito.

Soma Pia: Jux Azungumzia Kufanya Kazi na Megan Thee Stallion

Ngoma hiyo inazungumzia Jux kukubali kuvunjika kwa penzi lake na mpenzi wake wa zamani, na anamsifia kwa jinsi amepiga hatua kimaisha na hata kumpata mpenzi mwingine.

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania Bob Maneke ambaye alisimamia utengenezaji wa wimbo huo amefunguka kuhusu mchango wa Rayvanny kwenye utayarishaji wa ngoma hii. Kwa mujibu wa Bob Maneke, Rayvanny ndiye aliyetoa wazo la ngoma ya 'Sina Neno'.

Maneke alieleza kuwa Rayvanny pamoja na S2kizzy walikutana na Jux na kumpa wazo la kutoa ngoma hiyo. Rayvanny anadaiwa kuandika sehemu ya ngoma hiyo kabla ya Jux kuimalizia.

Soma Pia: Jux Aachia kanda ya wimbo wake 'Sina Neno'

Hapo awali, madai tofauti yaliibuka mtandaoni kuhusiani na mtunzi halisi wa ngoma hiyo.

'Sina Neno' ilipokelewa vyema na mashabiki na kufikia sasa takriban wiki tatu tangu kuchapishwa, imetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Rayvanny na Jux ni marafiki wa karibu mno si kwenye muziki tu bali kimaisha pia. Wawili hao walishirikiana kwenye wimbo wa 'Lala'. Ngoma hii imepata zaidi ya watazamaji milioni tano ndani ya miezi sita.

Leave your comment