Harmonize Aachia Kionjo cha Wimbo Wake Mpya ‘Single’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania na bosi wa lebo ya Konde Gang Harmonize amewaonjesha mashabiki zake kipande kidogo ya ngoma yake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram sehemu ya Instastory, Harmonize ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki amechapisha video fupi akiwa anaimba kipande kidogo cha wimbo huo.

Soma Pia: Chid Benz Asifu Rapa wa Kenya Khaligraph Jones kwa Kipaji Chake

Wimbo huo una mahadhi ya reggae, na ni ngoma ambayo wengi wameshuku kuwa inaweza ikaunda albamu yake ya ‘High School’

Ngoma hiyo ya Harmonize ameipa jina la ‘Single’ na mashairi yake yanamuongelea Harmonize ambaye kwa sasa hana mpenzi lakini anafuatwa sana na wasichana ambao wangependelea kuwa nae.

Soma Pia: Producer Bob Maneke Afichua Mchango wa Rayvanny Kwenye Wimbo wa Jux 'Sina Neno'

Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kuachia kionjo cha ngoma mpya kupitia Instagram. Agosti 15, siku kadhaa kabla hajaachia ngoma yake yake ya ‘Teacher’, Harmonize aliweka video fupi ambayo inadokeza kuhusu ujio wa ngoma hiyo ya Amapiano.

Mwaka 2021 umekuwa ni mwaka mzuri sana kwa Harmonize kwani tayari ameshatoa ngoma 10 ambazo zimebamba vilivyo kila sehemu ya Tanzania.

Kinachosubiriwa kwa sasa kutoka kwa Harmonize ni albamu yake ya ‘High School’ ambayo ametangaza kuwa iko mbioni kuingia sokoni ikiwa ni albamu yake ya pili tangu aachie ‘Afro East mwezi Machi mwaka 2020.

Leave your comment