Chid Benz Asifu Rapa wa Kenya Khaligraph Jones kwa Kipaji Chake

[Picha: Chid Benz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mkali kutoka Tanzania Chidi Benz amejitokeza na kumsifu rapa mwenzake Khaligraph Jones kutoka Kenya. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye runinga ya Wasafi TV, Chid Benz alisema anapenda mtindo wa Khaligraph wa kurap.

Alieleza kuwa mtindo wa Khaligraph ni wa kipekee na anafaa kuendelea nao bila kuubadilisha.

Soma Pia: Producer Bob Maneke Afichua Mchango wa Rayvanny Kwenye Wimbo wa Jux 'Sina Neno'

Chid Benz ambaye ni msanii wa kuheshimika ikijia katika mfumo wa Hip-Hop, alisema kuwa anakikubali kipaji cha Khaligraph Jones na anampenda kama msanii. Aidha, Chidi alifichua kuwa Khaligraph ni msanii ambaye hajaathiriwa na umaarufu kama wasanii wengine wengi.

Alisema kuwa msanii huyo amekuwa Tanzania mara kadhaa ila hajaweka picha mitandaoni kama vile wengine wangefanya.

"Kwa hivyo mimi ninamkubali, nampenda by the way, namuombea heri na namuombea aendelee kufanya kazi hivyo style yake anavyofanya," Chid Benz alisema.

Soma Pia: Nay Wa Mitego Aeleza Jinsi Usambazaji wa Albamu ya Alikiba Mtaani Umeathiri Mauzo Yake

Chidi Benz pia aliulizwa kauli yake kuhusu Khaligraph kuchukua baadhi ya mistari kutoka kwa wimbo wake. Chidi alisema kuwa anamuunga mkono Khaligraph. Alisimulia jinsi wakati mmoja alimsikia Khaligraph akisema kuwa anamuona Chid Benz kama mfano wa kuiga.

Chid Benz ni msanii ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania kwa muda mrefu sana. Amekuwepo tangu enzi za kale za bongo na hadi sasa bado sauti yake inasikika kwenye anga za burudani. Kwa sasa mashabiki wa Chidi Benz wanaendelea kusubiri albamu yake iliyopewa jina la 'Wa2 Wangu Album'.

Leave your comment