Tamasha la Nandy Festival Lapata Mafanikio Makubwa Kigoma

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nandy ameingia kwenye mitandao ya kijamii ambapo amechapisha ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wake baada ya tamasha la Nandy kufanyika Jumamosi huko Kigoma kwa mafanikio makubwa.

Mwimbaji huyo alikuwa na hisia katika taarifa yake na alihisi kunyenyekeshwa na idadi kubwa ya watu ambao walikuja kwenye tamasha. Tamasha la Nandy 2021 lilifanyika Kigoma ambapo mashabiki walijaza uwanja.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Nandy alikiri kuwa si rahisi kwa msanii kukusanya umati mkubwa kama huo. Kufanikiwa kwa tamasha la Nandy kuna maana kubwa sana kwake kama mwanamuziki katika tasnia ya burudani.

"Kigoma niko hapa natokwa na machozi. Sio rahisi ila mmenifuta jasho. Asanteni," Nandy alisema.

Wanamuziki wengine maarufu waliopanda jukwaani kuwaburudisha mashabiki wakati wa tamasha ni pamoja na Marioo, Babalevo, Linex, Stamina na wengine wengi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Wimbo Mpya ‘Nimekuzoea’ Toka EP ya ‘Taste’

Kilele cha tamasha hilo lilikuwa onyesho la Nandy pamoja na Alikiba. Wawili hao waliburudisha mashabiki kwa kiwango cha juu na walionekana kuwa na furaha zaidi.

Alikiba akiwa mmoja wa wanamuziki wanaofwatwa sana nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa wasanii wa mwisho kupanda jukwaani. Alikiba alikuwa hodari kwenye jukwaa kwa minenguo yake pamoja na nyimbo zake bora zaidi.

Nyota ya Nandy katika tasnia ya burudani ya Tanzania sasa inang'aa zaidi kuliko hapo awali.

Nandy kawaida huandaa sherehe hiyo kila mwaka.

Leave your comment