Nandy Atangaza Kumshirikisha Yemi Alade Kwenye Nyimbo 3

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mashuhuri kutoka Bongo Nandy amefunfuka kuwa yako na nyimbo tatu na msanii tajika kutoka Nigeria Yemi Alade.

Akizungumza na wanahabari sikuya Jumatano, Nandy alisema kuwa Yemi Alade amekua rafiki na msaidizi mkubwa katika kukuza sanaa yake.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Nandy alisema kuwa kufikia sasa, washarekodi nyimbo zaidi ya tatu pamoja ila ni swala la muda tu wa kuachia kazi hizo.

"Mimi na Yemi Alade tuna mazungumzo mazuri mpaka leo, ni dada mzuri kwangu ananishirikisha kwenye kila kazi yake anayotaka kutoa na hadi sasa tuna ngoma zaidi ya tatu ambazo tumeshazifanya hatujazitoa ni suala la muda tu,” Nandy alisema.

Itakumbuwa kuwa mnamo mwaka 2015, wawili hawa waliweza kukutana kupitia tamasha la Tecno own the stage lililokuwa nchini Nigeria. Wakati huo, Yemi Alade alikua miongoni wa majaji wa tamasha hilo la mziki.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Katika majadiliano hayo, Nandy pia alipata fursa yakuweka wazi mengi kuhusu mpenzi wake wa muda mrefu Billnass baada ya tetesi kusambaa mitandaoni kwamba wawili hao wameachana.

Kwanza alikanusha tetesi ya kuwa Bilnass alikua ameimba kumhusu yeye kwenye wimbo wake ‘Tatizo’.

“Wimbo wa Tatizo haunihusu mimi, watu wasikilize vizuri mashairi, Billnass kawaimbia vicheche na ma-ex zake ambao walimtenda coz ni mimi ndiye alinivisha pete!" alisema Nandy.

 

Leave your comment