Nandy Afunguka Kutupilia Mbali Tamasha Kadhaa Juu ya Malipo Duni

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika wa Bongo fleva Nandy amesema kuwa yeye na usimamizi wake wamelazimika kuacha tamasha nyingi kutokana na malipo yasiyo ya thamani yao.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Akizungumza katika hafla ya kuzindua ushirikiano wa tamasha lake la Nandy Festival, mwimbaji huyo amesema kuwa matarajio yake katika shows ni kupata hela zaidi ya milioni nane.

"Me na management yangu tumeshaacha shows kibao zile ambazo tunaona hazitupi thamani yetu, tumeshaacha show kibao za millions 8 au 7 kutokana na hatuioni thamani yetu, na show inapokuja vibaya upande wetu huwa tunaamini tu sio riziki yetu," alisema Nandy .

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kupitia tamasha la Nandy festival, Nandy amepanga kupeleka burudani kwa wakazi wa Kigoma, na miji zingine za Tanzania kasha avuke Kenya ambapo anapanga kuwa na show Nairobi na Mombasa.

Vile vile, Nandy alisema kuwa mipango ya miaka ijayo ni kupeleka tamasha hili hadi nchi zingine na wa sasa wapo wenye mazungumzo upande wa Burundi. Wasanii pia watakua wengi tofauti na miaka iliyopita.

 

"Mwaka huu Nandy Festival itafanyika kwenye mikoa 7 Tanzania, tutaenda pia Nairobi na Mombasa kwa upande wa Kenya lakini bado tupo kwenye mazungumzo kwa upande wa Burundi! Mwaka huu tutakuwa na list ya Wasanii wasiopungua 12 na surprises kibao humo ndani,” alisema Nandy.

 

Leave your comment