Nandy Atangaza Ujio na Taratibu ya Nandy Festival 2021

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutoka Bongo Nandy ametangaza ujio wa Tamasha kubwa litakalo beba jina lake ‘Nandy Festival’ mwaka 2021.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Akizungumza na wanahabari katika mkahawa wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi, Nandy alieleza kwamba tamasha litaanza tarehe tano mwezi Juni mwaka huu wa 2021 katika mkoa wa Kigoma.

Hili ni tamasha jipya kabisa katika bongo na limeandaliwa na Nandy kwa ajili ya kukuza na kutambua talanta mpya ndani ya mikoa saba nchini Tanzania na miji ya Kenya.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Hafla hii ya kila mwaka hufanyika katika majimbo anuwai ndani ya Tanzania. Hapo awali, tamasha hilo lilikuwa na wanamuziki wengi wa kike, lakini imekuwa na mseto wa kujumuisha jinsia zote kwa sasa akiwemo msanii marufu wa hip-hop Billnass. Nchini Kenya, Tamasha hilo litafanyika Mombasa na Nairobi.

“Nandy Festival mwaka huu inakuja kivingine na itafungua ukurasa mpya kwa vijana wote wenye uthubutu na hii sio yangu peke ni fursa ya sisi wote kama vijana nikimaanisha wasanii na wafanyabiashara hasa wadogo wadogo tutakao kutana nao mikoani kwenye tamasha,” alisema Nandy.

Tamasha hili likiwa la pili tangia Nandy kulizindua mwaka 2019 na kuenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya kuwafikia mashabiki wake nchini Tanzania.

Leave your comment