Nyimbo Mpya: Mbosso, Spice Diana Waachia Kanda ya Wimbo Wao ‘Yes’

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Wasafi Mbosso amechia kanda ya wimbo wake 'Yes' akimshirika Spice Diana kutoka Uganda.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Hii ni mojawapo ya kazi zake kutoka albamu yake ya “Definition of love…. “Yes” ni wimbo wa Harusi unaojibu swali kuhusu uhalisi wa mapenzi. Katika kuangazia maudhui ya ndoa wawili hawa wanaonyesha ufundi wao na ubunifu kwa kuelezea hisia zao kwa wimbo huu.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Mbosso anaanza kwa kueleza kuwa mapenzi hayagawanyiki na furaha yake ya kuwa na upendo ambao anaulinganisha na uzuri ulioko peponi ila yuko hapa duniani bado.

“Maagazi Jutoo, Mapenzi Hayagawanyiki, Nimepata Pumziko, Moyo Haupapatiki, Naionja Pepo Ingali Nipo Duniani (Duniani),Nalila Leo Na Kesho Penzi Lipo Siniani (Siniani), Nikunong’oneze Neno Zuri La Mapenzi…” aliimba Mbosso.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Jina ‘Kazi Iendelee’

Kanda hii ilitengeezwa kwa ufundi mkubwa kwenye maadhari ya msitu. Vile vile Spice Diana naye alitupa mazuri yake kupitia sauti yake kwa kuchanganya mistari ya Kiswahili na lugha ya Kiganda.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kwingineko katika mikato ya kanda hii tunamuona msakataji mkubwa wa Wasafi na mwenzake wakivunja uno kwa ufundi mkubwa.

Video hii ni ya Tatu kuto albamu ya Mbosso iilyotoka mwezi Machi na imepokelewa  vizuri na mashabiki wake Mbosso. Kufikia sasa “Yes” ina watazamaji zaidi ya laki sita kwenye mtandao wa YouTube huku video hii ikifanyiwa uelekezaji na Hascana.

https://www.youtube.com/watch?v=NClIIN8FgF4&ab_channel=Mbosso

Leave your comment