Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Jina ‘Kazi Iendelee’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii Zuchu na Rayvanny wameachia nyimbo mbili tofauti zenye mada sawa ‘Kazi Iendelee’.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Wawili hawa wameachia kazi hii kumsifia rais wa Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu. Katika wimbo wa Zuchu, anahadithia historia ya Rais Suluhu katika siasa kuanzia alipokuwa makamu wa Rais chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa Tanzania marehemu Dkt. John Pombe Magufuli alieaga mwezi mmoja uliopita.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea

Zuchu anatoa msimamo kuwa Rais Suluhu ndiye rais wa Tanzania, rais wake kama raia wa nchi nzima ya Tanzania na 'Kazi iendelee'.

https://www.youtube.com/watch?v=DVI01LmfY0I

Kwa upande wake Rayvanny amedondosha wimbo huu kwa kumsifia Rais Samia kama mama wa taifa na kama wananchi wanampa pongezi kwa kuhimiza kuwa 'Kazi iendelee'.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Awashirikisha Awilo Longomba na H Baba Kwa Wimbo Mpya ‘Attitude’

Katika mistari yake anaanza kwa kukumbuku za kifo cha marehemu rais Magufuli jinsi wanachi walivyohuzunika na kuvunjika mioyo kuhusu kifo cha rais huyo.

Rayvanny anaimba kuwa 'Kazi iendelee' katika sekta mbali mbali kwani aliye kwenye usukani anajali maslahi ya wananchi wake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux Adondosha Kanda ya Wimbo Mpya ‘Bado Yupo’

Nyimbo hizi mbili zinaonyesha hadhi na upendo kwa rais Suluhu katika kuendesha serikali yake. 'Kazi iendelee' ya Zuchu ilifanyiwa maandalizi na producer Moccogenius huku ya Rayvanny ikifanywa na Sound Boy wa Next level Music.

Kufiki sasa nyimbo zote mbili zinaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na kanda za nyimbo hizi zinatarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=rj3jXerJ1kA

Leave your comment