Nyimbo Mpya: Jux Adondosha Kanda ya Wimbo Mpya ‘Bado Yupo’

[Picha: Juma Jux Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa mziki aina ya RnB kutoka Tanzania Juma Jux ameachia kanda ya wimbo wake ‘Bado Yupo’.

Huu ni mojawapo wa nyimbo kutoka kwa albamu yake ‘The Love Album’ aliochia mwaka moja uliopita.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia EP Mpya ‘Wanibariki’ Yenye Mziki wa Injili

Wimbo huu umeachiwa kwa mfumo wa Acoustic ambapo Jux aliimbia kwenye studio za Better Session.

Katika ‘Bado Yupo’, Jux anaangazia hadithi ya mrembo aliyempenda na kwa sasa amevunjika moyo na hataki kupenda tena.

Anaimba anavyompenda na kusifia urembo wake na hapendi kumuona akiwa amesononeka kwa sababu ya mapenzi.

“Hello, habari gani? Hello oh ooh, unaitwa nani? Hello, uko gizani? Hello, kuna tatizo gani? Basi we nieleze Walipo kaza nilegeze You are so beautiful baby Hauendani na mawazo mama…” aliimba Jux.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Kanda hii haikuwa na kazi mingi katika maandalizi kwani video hii ilifanywa ndani ya studio.

Kufikia sasa ‘Bado Yupo’ ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya elfu kumi na saba. Hivi karibuni ameshirikishwa katika video mpya ya Rayvanny “Lala” ambapo alifanya kazi nzuri sana.

Uzoefu na sauti yake nzuri umefanya Jux kuwa mmoja wa wasanii anayetafutwa sana kwa ajili ya ushirikiana na wanamuziki wengine.

https://www.youtube.com/watch?v=YFslh7lp9Wg&ab_channel=AfricanBOY

Leave your comment