Nyimbo Mpya: Harmonize Awashirikisha Awilo Longomba na H Baba Kwa Wimbo Mpya ‘Attitude’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize ameachia wimbo wake mpya ‘Attitude’.

Katika wimbo huu Harmonize amewashirikisha Awilo Longomba na H Baba.

‘Attitude’ ni wimbo wa burudani ambapo Harmonize anaimba jinsi alivyotayari kuburudika kwa majigambo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Vile vile, anawaomba akina dada warembo wafurahi kwani hamna anayejua yatakayotendeka kesho.

“Nimekuja na hela mtaji wee, eh mtaji, Nipe pombe niinywe kama maji we, kama maji, Ukiniacha nitapanda bajaji we, ah bajaji, Sing today na today, Nobody knows tomorrow,All my beautiful ladies…” alimba Harmonize.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

H Baba kwa upande wake analeta ile ladha ya rhumba kwa ufundi wake mkubwa, huku awilo akileta ladha ya ule wimbo wake tajika “Coupe Bibamba” alioaachia miaka ya zamani kidogo.

Katika mistari yao wanasitizia umuhimu wa burudani katika maisha ya binadamu. Wimbo huu una mdundo mzuri unaompa mtu sababu ya kujiachia na kusakata densi kwa furaha.

Soma Pia:Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Wimbo huu uliandaliwa na Master Garzy. Kwa sasa ni wimbo unaokua kwa kasi kwenye mtandao wa YouTube na watazamji zaidi ya laki mbili ndani ya masaa tatu tangu kiuachiwa rasmi.

Kanda ya wimbo huu inatarajiwa wakati wowote sasa huku wengi wa mashabiki wakianza kulinganisha wimbo huu na ule wa Diamond Platnumz ‘Waah’.

https://www.youtube.com/watch?v=LHiHcIyFeI4&ab_channel=Harmonize

Leave your comment