Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muziki wa bongo unaendelea kunoga na wiki hii nyimbo za michambo kufuatia zogo la Harmonize na Rayvanny zimetamba zaidi. Hivyo katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano za bongo zinazovuma wiki hii:

Baikoko - Mbosso ft Diamond Platnumz

‘Baikoko’ ni wimbo wa densi unaolezea maana ya kipekee ya mapenzi. Wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwa kasi sana. Kwa sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni nne.

https://www.youtube.com/watch?v=hGqzvvbZnyQ

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Vibaya - Harmonize

Katika wimbo huu, anaangazia uhusiano wake wa awali na wapenzi wake. Katika ushairi wake, Harmonize anatumaini kutosemana vibaya na akina dada hao. Kwa sasa unawatazamaji zaidi ya milioni moja.

Nyamaza - Rayvanny

Wimbo huu unamlenga Harmonize kwa tuhuma za kujihusisha na mama na pia kumtaka mwanawe. Rayvanny naye anasema ni Bora Tembo angenyamaza au aombe radhi ya tuhuma hizo alizopata. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki tisa kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=FRhxiyDhoyw

SOMA PIA: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Lala - Rayvanny ft Juma Jux

Kutoka albamu ya ‘Sound From Africa’ Rayvanny aliachia wimbo ‘Lala’ yenye maudhui ya upendo. Jux kwa upande wake alionyesha ubabe katika mistari yake.Wimbo huu sasa ni mara ya pili unatokea kwenye orodha ya nyimbo bora na watazamaji zaidi ya milioni mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=s3kdjHUPlXA

Hayakuhusu - Ibraah

Ibraah wa Konde ganga aliamua kutupa michambo kwa Rayvanny kuhusu ugomvi aliokua nayo na Harmonize. Kwa bahati nzuri mashabiki walipokea wimbo huu kwa ukubwa na sasa una watazamaji zaidi ya laki saba.

Leave your comment