Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rayvanny ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: Rayvanny

Jina Halisi: Raymond Shaban Mwakyusa

Tarehe ya kuzaliwa: 22 Agosti 1993 (miaka 28)

Aina ya mziki: Bongo Fleva

Thamani ya jumla: Inakisiwa kuwa dola milioni moja hadi milioni tano

Soma Pia: Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Maisha ya mapema ya Rayvanny ilikuwaje?

Rayvanny alilelewa Mbeya Tanzania ambapo alisoma shule hadi siku zake za shule ya upili alipoonyesha kupenda muziki. Kulingana na yeye, wazazi wake hapo awali walikuwa wakimtaka asome na kuwa daktari, lakini shauku ya muziki ilizidi ile ya dawa.

Rayvanny alianzaje kazi yake ya muziki na lini?

Kipaji chake kiligunduliwa wakati wa Mashindano ya Freestyle mnamo 2011 huko Mbeya, ambapo aliibuka mshindi katika mashindano hayo na kupelekwa Dar es salaam, Tanzania.

Mnamo mwaka wa 2012, alijiunga na kikundi cha muziki kinachoitwa Tip Top Connection, ambapo alipata uzoefu zaidi katika kazi yake ya muziki na kushikamana na wasanii wengi. Mwaka wa 2015 aliamua kujiunga rasmi na lebo ya WCB Wasafi Records, ambayo iko chini ya uongozi wa Diamond Platnumz. Alitoa wimbo wake wa kwanza, ‘Kwetu’, mnamo 2016.

Je Rayvanny ana albamu?

Rayvanny ana albamu moja na EP mbili. Albamu yake inaitwa Sound From Africa Album ya nyimbo Ishirini na tatu,. EP zake ni kama vile; Flowers EP ya nyimbo nane na VannyBoy EP ya nyimbo nne.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Nyimbo Zake Bora

Number One

  • Kwetu
  • Pepeta
  • Tetema
  • I Love You
  • Amabako
  • Naogopa
  • Chuchuma
  • Vumilia
  • Ex Boyfriend
  • Natafuta Kiki

Rayvanny ana kazi za ushirikiano?

Rayvanny amepata fursa ya kufanya mziki pamoja na wasanii mbali mbali kwa nyimbo kama “Pepeta” aliomshirikisha Norah Fatehi, Number one akiwa na Zuchu na Remix yake akiwa na Muamerika Enisa, alishirikishwa kwa kazi za DJ Cuppy wa Nigeria miongoni mwa wengine wengi.

Rayvanny ana Tuzo Ngapi?

Mnamo 2016, Rayvanny aliteuliwa kwa Tuzo ya Muziki ya MTV Afrika katika kitengo cha “Breakthrough Act 2016”. Mnamo mwaka wa 2017 alichaguliwa pia kwa tuzo kadhaa za muziki, kama AEUSA ya Best New Talent, Tuzo ya Burudani ya Uganda kwa kitengo cha Best African Act, na Tuzo ya BET kwa Chaguo la Watazamaji wa Kimataifa (International Viewers’ Choice).

Mahusiano ya Rayvanny

Rayvanny alikua kwenye mahusiano awali na Fayhma ambae pamoja walijaliwa mtoto aitwaye Jadyden. Ila kufikia mwaka jana wawili hao waliachana kwa sababu zao. Kwa sasa Rayvanny anakisiwa kuwa na Paula Kajala binti wa aliyekuwa mpenzi wa Harmonize Fridah Kajala. Jambo ambalo limezua zogo kubwa kati ya wasanii Rayvanny na Harmonize.

Thamani Halisi

Kuhusu thamani yake Rayvanny anakisiwa kuwa na thamani ya dola milioni moja hadi milioni tano.

Leave your comment