Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Aslay na Marioo ni wasanii tajika kutoka Bongo na kwa sasa ndio wanaosifika kwa kazi zao za nyimbo za mapenzi za Kiswahili kutoka kanda ya Afrika Mashariki. katika nakala hii tunaangazia uwezo wa hawa wawili katika sanaa:

Soma Pia: Mdundo Mixes: Mixtape Tano Zinazovuma Nchini Tanzania (Pakua bila Malipo)

Uzoefu

Aslay ni msanii ambaye alianza mziki akiwa na umri wa miaka kumi na minne kabla ya kujiunga na kundi la Yamoto Bnad na kuachia kazi zilizoshabikiwa sana. Baada ya kundi hilo kusambaratika alijitokeza kama msanii wa Mziki wa RnB na alipokelewa vyema sana. Marioo kwa upande wake amepata umaarufu mkubwa mnamo mwaka 2017 baada ya wimbo wake ''Dar Kugumu" kupokelewa kwa kishindo. Hivyo wawili hawa wanashindana katika uzoefu na kila mmoja na nguvu zake kimziki.

Tuzo

Asay kwa uzoefu wake katika mziki hana Tuzo ya kibinafsi ila moja tu ya wakati akiwa kwenye Yamoto Band ya Kundi Bora zaidi kwenye tamasha la African Entertainment Awards, USA. Marioo pia hajashinda tuzo zozote za mziki ila kuna tumaini kubwa kwa msanii huyu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video Yake Mpya ‘For You’

Albamu

Aslay hana albamu ila ana EP kwa jina “Kipenda Roho” aliochia mwaka uliopita kabla ya kupotea kwenye mziki kwa muda mfupi. Mwaka huu mashabiki walikua na matumaini kuwa ataachia albamu mpya sasa ni kusubiri tu. Marioo kwa upande wake pia hana albamu hata moja ila ameachia nyimbo nyingi sana katika kukuza sanaa yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Wimbo Mpya 'Vumilia'

Usajili na Utazamaji kwenye mtandao wa YouTube

Kufikia sasa Aslay anawasajili zaidi ya laki saba kwenye mtandao wa YouTube huku Marioo akiwa na zaidi ya laki Tatu. Aslay ana jumla ya watazamilioni milioni 160,020,548 ihali Marioo ama milioni 40,995,477 kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Amapiano: Mdundo Unaobadilisha Mitindo ya Muziki wa Bongo Fleva

Wafuasi Kwenye Instagram

Kwenye mtandao wa Instagram, Aslay ana wafuasi milioni nne nukta sita ilhali Marioo ana wafuasi milioni mbili nukta nne. Mtandao wa Instagram ukiwa na umuhimu mkubwa kwa wasanii wa Tanzania katika kusambaza kazi zao mpya.

Leave your comment