Rayvanny Awashukuru Wasanii Waliomkuza Kimuziki Akizindua Lebo Yake ‘Next Level Music’

[Picha: Wasafi Media]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu Rayvanny amezindua rasmi lebo yake mpya kwa jina ‘Next Level Music’. Katika sherehe hio ya uzinduzi, Rayvanny aliwapa heko wasanii waliomshika mkono na kumsaidia kunawiri kimuziki.

Kama anjia ya kuwapa heshima na thamani waliomshika mkono, Rayvanny ameweka picha zao kwenye kuta zake za studio. Picha hizo ni za waanamziki na hata uongozi mzima wa WCB kwa kukuza talanta yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Kwenye picha ya kwanza Rayvanny ana Mtangazaji wa Clouds Media Fetty. Rayvanny alisema Fetty alipendezwa na kuimba kwake kuliko kurap kama alivyokua ameanzia. Hivyo, aliona ni heri kumpa DJ Fetty heshima yake.

Picha ya pili ni ya Madee ambaye Rayvanny alimtaja kama kaka na baba mkubwa kwa kumlea kimziki na kumfanya kuwa na ujasiri wa kufanya tamasha mbali mbali.

Soma Pia: Mixes Tano Bora za Kupakua Kwenye Mdundo Wiki Hii

Kisha akafwata Babu Tale ambaye Rayvanny alisema alimsaidia kuwa mtu wa heshima na kukuza sanaa yake. Kisha akaja Meneja Mkubwa Fella, huyu naye Rayvanny alielezea kuwa alipata kumuamini wakati akiwa na lebo ya Mkubwa na wanawe na bandi ya Yamoto.

Soma Pia: Rayvanny Kutambulisha Lebo yake Mpya ‘Next Level Music’

Kisha akaonyesha picha ya Meneja Sallam Mendez na kusema yeye ni mtu anayempambania sana, hivyo yeye ni familia. Alimalizia kuionyesha picha ya bosi wake Diamond Platnumz ambaye alisema kuwa ni mfano wa kuigwa na pia amekua kigezo kikubwa katika sanaa yake.

Aliongeza kuwa ni Diamond aliyemfunza jinsi ya kujiendesha katika biashara ya mziki. Vile vile aliongeza kuwa Simba alishinda kumkumbusha kutochoma daraja anazotumia kama kivuko cha maisha.

Leave your comment