Rayvanny Kutambulisha Lebo yake Mpya ‘Next Level Music’

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anaefanya vizuri kwa sasa na Album yake ya “Sound from Africa” Rayvanny ametambulisha rasmi jina na logo la lebo yake mpya 'Next Level Music.'

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny amepost picha yenye logo ya lebo hiyo na kuandika "Ilikuwa ndoto Next Level Music #NLM.”

Soma Pia: Mixes Tano Bora za Kupakua Kwenye Mdundo Wiki Hii

Ikumbukwe katika moja ya mahojiano, bosi wake Rayvanny Diamond Platnumz alithibitisha kuwa hajawafungia wasanii wake fursa kuanzisha lebo zao, ila tu zitakuwa kuwa chini ya WCB.

Awali, Diamond alishasifia kuwa studio ya Rayvanny mojawapo ya studio kali ambazo amewahi kuziona Tanzania.

“Sijui kama nafaa nizungumze lakini Rayvanny anaanzisha lebo yake muda si mrefu …..Lebo yake kubwa sana . Nilikua naangalia studio yake naamwambia eiy Rayvanny Studio yako hii kubwa eiiy…Kwa sasa hivi akiiposti ndio itakua studio namba moja…” alisema Simba.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Navy Kenzo Waachia Video Mpya ‘Nisogelee’

Vilevile, Diamond Platnumz ametangaza kuwa na sherehe hii leo katika lebo hiyo ikikisiwa kuwa uzinduzi rasmi wa lebo hiyo mpya.

 Huku akisema watakaohudhuria ni waalikwa tu. Kwa sasa ni kusubiri taarifa kutoka kwake Rayvanny kutambulisha lebo yake NLM rasmi na iwapo kuna wasanii ambao atazindua hivi karibuni.

Rayvanny sasa ni msanii wa kwanza kwenye labl ya Wasafi kumiliki label yake binafsi huku akiendelea kufanya kazi na label yake.

Leave your comment