Mixes Tano Bora za Kupakua Kwenye Mdundo Wiki Hii

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Tunapoanza wiki mpya katika mwezi huu wa Machi 2021, Mdundo umekuandalia mixtapes tano mpya za kukusisimua na kukuchanagamsha unapoendelea na shughuli zako.

Mixtape hizi zina mchanganyiko wa wimbo moto moto kutoka kwa wasanii tajika eneo la Afrika Mashariki.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Mpya za Muziki Bora Machi 2021

Hii hapa orodha ya mixtape tano mpya zilizo kwenye Mdundo Tanzania unazofaa kupakua na kusikiliza mwezi huu:

Bongo Mix March 2021 Vol 1

Mixtape hii ni yenye maudhui ya mapenzi na ina nyimbo kutoka kwa wasanii kama vile; Aslay, Darassa, Ruby na Nadia Mukami. Ijapokuwa mwezi na siku ya wapendanao ilishapita, bado unaweza kusikiliza nyimbo hizi pamoja na mpenzi wako ili kuwachangamsha na kusisimua mapenzi yenu.

DJ Bee East African Mix

Hii n mixtape yenye nyimbo bora kutoka kwa wasanii tajika eneo la Africa Mashariki. Nyimbo hizi zina mdundo wa kusisumua na ni zeny maudhui ya kudensi na kufurahia maisha. Iwapo unataka kujipa raha mwenyewe, basi pakua mixtape hii kwenye mtandao wa Mdundo Tanzania. Wasanii walioshirikishwa ni kama vile; Nyashinski, Shebah, Kelechi Africa na Willy Paul.

DJ Bee East African Mix Vol 2

Mixtape hii ina nyimbo zenye midundo ya kutumbuiza na kufurahisha kutoka eno la Afrika Mashariki. Nyimbo zilizo kwenye mixtape hiiniya maudhui ya mapenzi. Wasanii walioshirikishwa ni kama vile; Willy Paul, Otile Brown, Vinka, Meddy Aslay na wengine wengi.

International Women’s Day Edition

Mixtapee hii iliandaliwa ili kuwasherekea wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwenye sanaa ya muziki. Tarehe8 mwezi wa Machi huwa siku ya wanawake duniani, hivyo mixtape hii iliandaliwa ili kuambatana na siku hio. Wasanii walioshirikishwa ni kama vile; Zuchu, Nandy na Duduke miongini mwa wengine.

International Women’s Day Edition Vol 2

Mixtape hii pia ni ya kuwasherehkea wasanii wa kike kutoka bara Afrika wanaofanya vizuri kimuziki. Mixtape hii inamchanganyiko ya wimbo kutoka Nigria, Kenya na Bongo. Wasanii walioshirikishwa ni kama vile;Yemi lade, Zuchu, Maua Sama na Ssaru.

Leave your comment