Nyimbo Mpya: Navy Kenzo Waachia Video Mpya ‘Nisogelee’

[Picha: Navy Kenzo Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Wasanii tajika kutoka Tanzania Navy Kenzo wameachia kanda ya wimbo wao mpya kwa jina ‘Nisogelee’.

Huu ni wimbo wa densi wa kupendeza ambapo waimbaji hawa wanapeana changamoto kucheza bila uoga.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tanzanian Men All Stars Waachia Wimbo ‘Superwoman’

‘Nisogelee” una mbwembwe za kufurahisha mtu yeyote anayeulewa mziki.

“Wapenda mambo ya pwani limbwata utanasa! Vurugu mfano wa tsunami kigoli matata, Nalamba mpaka jokeri mchezo wa karata,utamau mpaka usogoni ya swadakta…” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Ukitazama video hii, utapendezwa na ubunifu wa usakataji na dnsi zilizotumika.Kwingineko, mdundo wa wimbo ni ule wa kutoka Afrika kusini Amapiano. Mdundo huo kwa sasa umeanza kutumiwa na wanamziki mbali mbali barani Afrika kwa ajili ya kuendeleza mziki wa bara hili.

Siku ya Wanawake Duniani: Nyimbo Tano Zinazowasifia Wanawake Kutoka Bongo

“Nisogele” ni kazi ya kwanza Navy Kenzo mwaka huu wa 2021 baada ya albamu yao ya ‘Story of the African Mob’ kufanya vizuri hapo mwaka jana.

Kufikia sasa, albamu hiyo imepata zaidi ya wasikilizaji zaidi ya milioni sita kwenye mitandao ya kucheza mziki. Video hii imepokelewa vizuri huku ikipata watazamaji zaidi ya elfu hamsini na sita huku kanda hii ikiandaliwa na mwelekezaji Director Ivan.

https://www.youtube.com/watch?v=WkroWpr7Bfg&ab_channel=NavyKenzo

Leave your comment