Nyimbo Mpya: Tanzanian Men All Stars Waachia Wimbo ‘Superwoman’

[Picha" Wasafi TV Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Wasanii wa kiume mashuhuri Tanzania wameachia wimbo mpya kwa jina ‘Superwoman’.

Wimbo huu ni maalum kwa ajili ya kusheherekea siku ya wanawake itakayoadhimishwa tarehe 8 mwezi huu wa Machi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Jux Zinazovuma 2021

Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa: Wanawake katika uongozi: Kufikia siku zijazo sawa katika ulimwengu wa COVID-19.

Hivyo, ‘Superwoman’ ni wimbo wa kuunga na Kuthamini harakati na mchango wa wanawake katika jamii.

Wimbo huu ni toleo la pili. ‘Superwoman’ ya kwanza ilifanywa mwaka jana na wasanii wote wa kike kutoka Tanzania. Katika wimbo wa mwaka huu, wasanii husika ni kama vile Diamond Platnumz, Belle 9,Juma Jux, Marioo, Dulla Makabila, Rayvanny, Lava lava, Mbosso, BabaLevo, Joel Lwaga, Gnako, Barnaba na Madee.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia EP Mpya ‘Wanibariki’ Yenye Mziki wa Injili

“… Upendo wako, heshima yako dunia nzima mfano hakuna, You are the Superwoman…” aliimba Belle 9.

Wasanii hao kumi na tatu walikua na fursa ya kumsifia mwanamke. Ukiskiliza wimbo huu unapata kufuhishwa na heshima wasanii hawa wanayowamiminia akina dada.

Ni muhimu kutambua mchanganyiko wa sauti na hata mdundo ambapo Dulla Makabila alifunga wimbo huu kwa mdundo wa singeli . Wasanii hao wanaamini kuwa mwanamke anajiweza katika njia mbali zikiwemo uongozi, biashara miongoni mwa vingine vingi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘For You’

Kufikia sasa wimbo huu umepokelewa vizuri sana nchini Tanzania haswa katika kampeni ya Siku wanawake inayoangazia usawa wa watu wa jinsia zote. Mdundo wa wimbo huu uliandaliwa na Producer mkubwa Lizer Classic huku kanda yake ikitarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=BTyUxNW162k&ab_channel=WasafiMedia

Leave your comment