Siku ya Wanawake Duniani: Nyimbo Tano Zinazowasifia Wanawake Kutoka Bongo

[Picha: DJ Mwanga]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Tarehe nane mwezi Machi huwa tarehe ya kuadhimisha siku ya wanawake ulimwenguni. Hivyo Tanzania imekua kwenye kipaumbele katika kuwapa wanawake hadhi ya uongozi na hata biashara. Wasanii wengi wametumia talanta yao kusifia uwezo wa mwanamke katika jamii. Hizi hapa baadhi ya nyimbo hizo:

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Mpya za Muziki Bora Machi 2021

Super Woman – Tanzanian All Women Stars

Huu ni wimbo wa kusifia taadhima ya mwanamke ambaye akipewa nafasi yake katika jamii ana uwezo wa kufanya lolote. Wimbo huu ulifanywa na wasanii tajika wakike nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=UaamB7o--Ck&ab_channel=WasafiMedia

Super Woman - Tanzanian All Men Stars

‘Superwoman’ ni wimbo wa kuunga na kuthamini harakati na mchango wa wanawake katika jamii. Wasanii hao kumi na tatu walikua na fursa ya kumsifia mwanamke. Ukiskiliza wimbo huu unapata kufuhishwa na heshima wasanii hawa wanayowamiminia akina dada.

https://www.youtube.com/watch?v=BTyUxNW162k&ab_channel=WasafiMedia

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tanzanian Men All Stars Waachia Wimbo ‘Superwoman’

Lady with Confidence – Khadija Kopa

Huu ni wimbo wa kumsifia mwanamke mwenye sifa za kipekee. Anaangazia mwanamke wa kujiamini katika maisha. Hapa Kopa alifanya wimbo huu kuwapa wanawake nguvu ya kujiamini.

https://www.youtube.com/watch?v=T2HNH-znzoI&ab_channel=AfrichaEntertainment

Mama - Benpol ft Goodluck Gozbert

Ben Pol alimshirikisha msanii wa injili Goodluck Gozbert katika wimbo wa ‘Mama’ ambapo wawili hao wanamshukuru mama yao kwa kuwalea na kuwatunza katika maisha yao yote.

https://www.youtube.com/watch?v=Nvb7Q39PUFg&ab_channel=BenPol

Mama - Yamoto Band

Tangu enzi, mama ni mtu muhimu sana, na amekuwa akiimbwa na kupata wasifu mkubwa toka kwa wasanii mbali mbali ikiwa ni njia ya kuonyesha kumthamini na kuwaheshimu wanawake.Hii ndio sababu vijana hao waliona bora kumsifia mama.

https://www.youtube.com/watch?v=F9-3gZpK0zQ&ab_channel=MkubwanaWanawe

Leave your comment