Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Albamu yake Mpya ‘Definition of Love’

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Baada ya pilkapilka zake za kutafuta maana ya mapenzi, hatimaye Mbosso ameachia albamu yake ya ‘Definiton of love’.

Hii ni albamu iliyosubiriwa sana na mashabiki huku matarajio yakiwa ya juu zaidi. Hivyo Mbosso amelazimika kuiachia albamu hiyo leo tarehe tisa badala ya tarehe kumi na tatu Machi ilivyotarajiwa awali.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

‘Defition of Love’ in albamu ya msanii Mbosso ya kwanza tangia aingie kwenye lebo ya wasafi miaka mitatu iliyopita.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Collabo 5 Zake Diamond Zinazovuma Bongo [Video]

Kwenye albamu hii kuna nyimbo kumi na mbili na mbili za ziada mbazo wanaziita “Bonus tracks”- yaani zawadi ya mashabiki.

Vilevile Mbosso amewashirikisha wasanii mbali mbali wakiwemo kutoka Tanzania ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Njenje wa Kilimanjaro Band, Darassa na Babalevo kisha Spice Diana wa Uganda alafu Liya na Mr Flavour wa Nigeria.

Nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni kama vile:

Mtaalamu

Kwenye wimbo huu, Mbosso atupa maana yake ya mapenzi kwa kusema kuwa amepata “Mtaalamu” wa Mapenzi.  Hivyo huyu ni wa kuonyesha upendo na si wakujilizaliza wakati panapo shida.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Mpya za Muziki Bora Machi 2021

Karibu ft Diamond Platnumz

Huu ni wimbo wa kuelezea mapenzi ya mzazi kwa mwanae. Mbosso na Diamond Platnumz wanaonyesha mapenzi ya dhati kwa watoto wao huku wakionyesha umuhimu wa kuwakaribisha katika ulimwengu.

Your Love ft Liya

Hapa Mbosso amemshirikisha Liya wa Nigeria na wawili hao wanaangazia mapenzi yao yalivyonoga.

Nyimbo zingine kwenye album hio ni kama vile :Kiss Me, Pakua Ft Rayvanny, Kadada ft Darassa, Yes ft Spice Diana, Nipo Nae, Limevuja, Baikoko ft Diamond Platnumz, Yalah, Mselelekoh, Sakata ft Mr Flavor, Tulizana ft Njenje wa Kilimanjaro band.

Albamu hii ilifanywa kwa ubunifu wa producers S2kizzy, Lizer, Trone, Abbah Process, Abby Daddy, Kapipo, Nusdur Venum na Artin Pro. Kufikia sasa, albamu hii imepokelewa vizuri na inapatikana katika mitandao yote ya kucheza mziki.

https://www.youtube.com/watch?v=UxxucBEFHY4&list=PLVTehZ7qhaEMOlDRqi9eqFUvMGJ89spR1&index=10&ab_channel=Mbosso

Leave your comment