TANZANIA: Mzee Kassim Mapili afariki dunia.

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Mzee Kassim Mapili afariki dunia. Taarifa za kifo cha Mzee Mapili zimeenea baada ya kutokuonekana nje ya nyumbani kwake kwa muda wa kipindi kirefu. ndipo mlango wa chumbani kwake u;ipovunjwa na kukuta Mzee Mapili hatunae tena. Inasemekama kifo chake kimejulikana usiku wa jana baada ya majirani kutomuona kwa muda wa siku mbili nzima na kutia mashaka, ndipo walipoamua kuvunja mlango wa nyumba yake na kukuta mwili wake.

Majirani wa Mzee Mapili wamesema mara ya mwisho kumuona mkongwe huyo ambaye alikuwa akiishi peke yake nyumbani kwake, ni juzi ambapo waliangalia pamoja mtanange kati ya tinu za Arsenal na Barcelona. Shuhuda mmojawapo amesema mwili hauko katika hali nzuri, na jitihada za kuwatafuta ndugu zake zinaendelea. Mzee Mapili alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo kabla ya kifo chake.

Taarifa kutoka kwa Rais wa shirikisho la muziki nchini, Ado November imesema:

Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili. Atakumbukwa kwa kibao cha ‘Napenda Nipate Lau Nafasi na Rangi ya Chungwa. Mazishi ya leo Ijumaa 26/02/2016 saa kumi jioni Kisutu. Maiti haipo ktk hali nzuri daktari kashauri azikwe haraka. Msiba upo mtaa wa Magomeni na.23 Mapipa. Tujitokezeni wapendwa kama ungependa kujiunga nasi kwa mchango basi tuma rambirambi kwa Hassan Msumari-Katibu Mkuu Chamudata, namba zake 0717340533, Addo November – Rais Shirikisho la muziki Tanzania – 0744150000.

Leave your comment