TANZANIA: Kaa tayari kwa kolabo kati ya Bella na Weusi.!

 

King Dodoo ambaye ni manager wa msanii Christian Bella amezungumzia wimbo mpya wa msanii huyo na kundi la Weusi, na kwanini Weusi? Aina ya wimbo na maana yake, pia unatoka lini?

Akiongea na mtangazaji, Smashratino wa Radio FM ya Dodoma, King Dodoo alisema;

“Naongea kama meneja wa Bella kutoka na wimbo mpya wa Bella na Weusi. Unajua muziki ni kufurahisha watu na ndio maana Bella ameamua kufanya kazi na Weusi na kuwafanya mashabiki pia wa Hip hop wapate ladha tofauti na kuonyesha kuwa bella anaweza kumix Dance na hip hop na pia anaweza kufanya kazi na kila msanii. Nafikiri wiki ijayo wimbo utakuwa tayari unaitwa ‘Penzi Langu’”.

“Maana halisi ya wimbo ni kwamba watu wengi sana wanapenda kuiga katika mapenzi badala ya mtu kukaa na mpenzi wake akatulia unamkuta wanaiga maisha ya katika mitandao maana maisha ya mtandao kila mtu anaishi maisha ya kishua nafikiri hiyo ndo ladha ya huo wimbo”, aliongeza Dodoo.    

Leave your comment