TANZANIA – Nikiachana na muziki nahamia kwenye siasa – Diamond

 

Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Tamaduni na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.

“Kwa hivi sasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye, akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo”.

“Kile nakiweza kabisa kwasababu mimi ukiniambia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa waziri, nikavifanya na vikawa na mendeleo. Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri wa Habari, Tamaduni na Michezo na kuboresha vitu”, aliongeza Diamond.

Diamond ambaye hakusema kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu

uliomuingiza Rais Mgufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.

Leave your comment

Top stories