EXCLUSIVE (TANZANIA) – Hii hapa kauli ya Ali Kiba kuhusu Diamond kupitisha video za wasanii wa Bongo kuchezwa MTV Base

Hivi karibuni msanii Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa kituo cha kimataifa, MTV Base huwa wanampigia kuidhinisha video yoyote inayotumwa kwenye kituo hicho kutoka Tanzania ili azitolee maoni ili zipitishwe au la. Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa muziki wakiwemo wasanii wenyewe.

Kati ya wasanii waliozungumzia kuhusu kauli hiyo ni pamoja na Ali Kiba, ambaye ikumbukwe kuwa video zake hazionyeshwi na kituo hicho, kitu kinacholeta utata kutokana na tofauti kati yake na Diamond.

“Nitawaambia ukweli ambao unawahusu kama ni kweli watakua wanakosea MTV haikai sawa na sidhani kama ni kweli”, aliongea Ali Kiba kupitia XXL ya Clouds Fm alipoulizwa maoni yake kuhusu swala hilo.

“Yaani haikai sawa na sidhani kama ni kweli, kwasababu watakuwa hawako fair, hajabeba talent ya kila mtu (Diamond), kila mtu ana kipaji chake na kila mtu ana haki ya kuonyesha kipaji cha kazi yake. Unajua kila mtu anafanya biashara ya muziki saizi, sio mtu anafanya masihara unapoona mtu anafanya video yake anagharamikia unajua haipendezi, kwahiyo sidhani kama ni kweli”, Alisema Ali Kiba.

Kauli hiyo aliitoa Diamond alipokuwa akijieleza jinsi wasanii wanavyomtupia lawama kuwa anawanyima connection za kung’ara kimataifa, “Mimi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mimi najitaidi kuwasaidia wenzangu ili tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mimi ndo huwa nasababisha”, alisema Diamond kupitia Papaso ya TBC Fm.

“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwasababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mafano MTV wenyewe wakipokea video toka kwa msaniiyeyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? Tuicheze ngoma yake ama? Mimi huwa nasema anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu” Alisema Diamond.

Leave your comment

Top stories