EXCLUSIVE (TANZANIA) – Watanzania kuvamia ukurasa wa Instagram wa Tekno wa Nigeria kwa comment za RIP.

 

Tukio la msanii wa Bongo Movie Steven Kanumba linaendelea kumwandama aliyekuwa mpenzi wake Elizabeth Michael ‘Lulu’, kutokana na tabia za baadhi ya Watanzania kuendeleza tabia isiyokubalika ya kumkejeli mwanaume yoyote anayesemekana kuwa na uhusiano nae kuwa kifo kinamnyemelea.

Tabia hiyo imejitokeza pia kwa muimbaji wa Nigeria, Tekno aliyedaiwa kuwa na uhusiano naye baada ya kupiga picha naye kwenye show aliyoifanya siku ya mwaka mpya jijini Dar. Hata hivyo Lulu alikanusha taarifa hizo kuwa ni za uzushi kwakuwa hakuna kinachoendelea kati yao.

Tangu hitmaker huyo wa Nigeria arudi nchini kwake amekuwa akipata comments nyingi kutokana na uzushi kuwa amenasa kwenye ulimbo wa Lulu, lakini kilichokuja kumchukiza zaidi ni comments za RIP zilizompelekea kufuta picha zake zote na kuandika ujumbe mrefu kueleza Wanigeria na wengine wasioelewa sababu za comments za RIP kwenye ukurasa wake.

Haya ndiyo maelezo aliyoyaandika Tekno na baadae kuyafuta;

“Kwanza kabisa, ninamsamehe kila mmoja wenu aliyecomment RIP kwenye ukurasa wangu

Kwa familia yangu, marafiki, bloggers na wote mliokuwa mkinipigia simu kuniuliza hizo comments za RIP zinamaanisha nini, kuna wanaosema nimetenda kosa la jinai nilipokuwa Tanzania! Lol.

Nilichokifanya mimi ni kupiga picha na msichana mrembo wa Tanzania sitamtaja jina lake. Kilichotokea ni kwamba wanaume wachache amba waliwahi kuwa na uhusiano nae walifariki, kama wanavyosema!

Kwahiyo hawa watu wanaocomment RIP wanaamini kuwa nina uhusiano nae kwasababu ya picha niliyopost Instagram ya mimi nay eye (Lulu), hivyo na mimi nitakufa, Wow, Inafurahisha.

Kwanza, nyie ni nani wa kuhukumu maisha yake?

Pili, nyie ni nani kucomment R.I.P kwenye ukurasa wangu ..

Mungu tusamehe na utuangalie wote. Sasa mmefahamu”.

 

Leave your comment