Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aungana Na Ntoshi Gazi Kwenye 'Chuu'


[Image Source: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pakua Mixes Mpya Kila Siku Ndani Ya Mdundo

Kaulimbiu ya Singeli To The World inaendelea kufanyiwa kazi na wasanii wa Singeli na hii ni baada ya Meja Kunta, ambaye kwa sasa amesainiwa kwenye moja ya record labels kubwa hapa Bongo Bxtra Records kuachia ngoma yake mpya ya kuitwa Chuu.

Kwenye Chuu, Meja Kunta amemshirikisha Baba Levo pamoja na msanii kutoka Afrika Kusini Ntoshi Gazi ambaye ameongeza vionjo vya Amapiano kwenye ngoma hii ya Singeli ambayo imetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa Singeli kwenye tuzo za TMA 2023 Eyoo Kenny.

Chuu ambayo ndani yake Meja Kunta amelenga kuchangamsha mashabiki hasa wanaopenda kula bata na kustarehe ni ngoma ya kwanza ya Singeli kushirikisha msanii wa kimataifa hivyo kuandika historia mpya kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

Collabo hii kutoka kwa Meja Kunta inakuja miezi michache tangu mkali huyo wa Singeli asainiwe na lebo ya Bxtra Records inayomilikiwa na mtayarishaji wa muziki Hermy B, lebo ambayo pia inasimamia kazi za wasanii wengine ikiwemo Country Wizzy, Jaivah pamoja na Cherry.

Kando na Chuu, kwa mwaka 2023, Meja Kunta alitoa ngoma tofauti tofauti ikiwemo Ushali, Demu Wangu Remix akiwa na Marioo pamoja na Tabia Mbaya.

https://youtu.be/7iRqpa1emps?si=yrYWbyPJ74I3Hzyt

 

 

Leave your comment