Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Amepotea: Mbosso Kivingine Na Ngoma Mpya
12 May 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi-Charles Maganga
Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii
Baada ya ukimya wa takriban miezi mitano tangu aachie EP yake ya kuitwa “Khan” msanii Mbosso kutokea WCB amerudi tena na ngoma mpya kabisa ya kuitwa “Amepotea”
Ikumbukwe kuwa Mbosso wiki chache zilizopita, alishinda tuzo moja katika Tanzania Music Awards kama Msanii Bora Wa Bongo Fleva kwenye tuzo hizo.
Kwenye ngoma yake hii mpya ya kuitwa “Amepotea”, Mbosso anachukua nafasi ya mwanaume anayetafutwa kwa hali na mali na familia yake baada ya yeye kutoroka na kuhamia kwa mpenzi wake ambako anapewa mahaba mazito.
“Amepotea” imetayarishwa na S2kizzy ambaye ni mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania ambaye ameshafanya kazi na wasanii wakubwa mbalimbali huku video ikiwa imetayarishwa na Director Ivan.
Weekly Top 10 songs

Inama4:58
ONLY YOU JESUS5:44
Bikyaganye3:29
Mshamba2:44
Daddy2:50
Sissa3:37
Eazzy Ft Way Dee2:59
Alaska2:29
Come Alive3:32
Deep House BLACK5:35
Top stories
- KACHUMBALI ARMY
08 October
- KACHUMBALI ARMY(Kiswahili)
08 October
- My incoming songs
09 October
- USINIACHE
09 October



Leave your comment