NYIMBO ZA TANZANIA ZINAZOFANYA VIZURI KENYA WIKI HII.
5 May 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi-Charles Maganga
DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3
Kwa muda mrefu sasa nyimbo kutoka nchini Tanzania zimekuwa ni burudani pendwa kwa mashabiki wa muziki nchini Kenya na ndio maana wasanii wengi kutoka Tanzania mara nyingi hupaita Kenya “Second Home” yaani taifa lao la pili.
Kwa wiki hii mambo yamendelea kuwa bomba kwa wasanii wa Tanzania na hii ni baada ya baadhi ya nyimbo kutoka Bongo kuwepo kwenye orodha ya nyimbo zinazofanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Kenya.
Kutoka kwa wasanii kama Zuchu, Kontawa na wengineo hizi hapa ni nyimbo kutoka Tanzania zinazofanya vizuri nchini Kenya kwa wiki hii:
Zuchu - Utaniua
Video ya Utaniua bila shaka imepokelewa vyema nchini Kenya kwani kwa sasa inashika namba moja kwenye mtandao wa Youtube. Ndani ya siku tatu pekee wimbo huu tayari umeshakusanya views takriban 1.9 Milioni.
Namficha - DJ Joozey Ft Harmonize
Tangu kuachiwa kwake, Namficha imekuwa ngoma pendwa kwa wapenzi wa muziki mzuri na kwa wiki hii imeshika nafasi ya pili kwenye orodha ya nyimbo za Tanzania zilizotazamwa zaidi nchini Kenya.
Forever - Rayvanny
Video ya “Forever” ya kwake Rayvanny akiwa na Fahyma inaenda kufanya vizuri sio Tanzania lakini pia nchini Kenya ambapo kufikia imeshakusanya views zaidi ya Milioni ikiwa na takriban mwezi mmoja tu tangu kuachiwa kwake
Ananipenda - Platform Ft Marioo
Ananipenda ya kwake Platform na Marioo kwa mara nyingine imedhihirisha chemistry nzuri waliyonayo wasanii hawa wawili kiasi cha kupokelewa vizuri sana huko nchini Kenya kwa wiki hii.
Dunga Mawe - Kontawa
Kontawa, mshindi wa Tuzo za Tanzania Music Awards kama msanii bora wa kiume kwa mwaka 2023 ni fundi haswa na ndio maana wimbo wake wa “Dunga Mawe” umekuwa ndio wimbo wa Hip Hop Kutoka Tanzania unaofanya vizuri zaidi nchini Kenya kwa wiki hii mtandao wa Youtube.
Top Artists: Lucky Dube, JUX, Christina Shusho, Marioo, Ukhty Dyda, Victony, Ayra Starr, Best Naso, Jay Melody
Quick Links
Daily Mixes
DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST TZ MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST BEST SONGS 2022 MP3
DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3
DOWNLOAD LATEST MUSIC ALBUMS/EP MP3
DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF 2023 MP3
DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3
DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF THE WEEK MP3
DOWNLOAD LATEST AFRICAN MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST GHANA MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST KENYA MUSIC MP3
Leave your comment