Ubashiri Mechi Ya Liverpool Vs Chelsea EPL- Mdundo Alt

[Picha: The Sun]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Majoogo wa London Liverpool watavaana na wababe kutokea Stanford bridge Chelsea siku ya Jumamosi katika uwanja wa  Anfield ukiwa ni mchezo wa ligi kuu Uingereza, Liverpool wakiwa wenyeji.

Katika mchezo huu timu zote mbili zitakuwa zikihangaika kutafuta alama tatu kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri katika ligi haswa baada ya kuandamwa na majeruhi na kuzifanya zikose wachezaji muhimu.

Liverpool wakiwa nafasi ya tisa wanapitia wakati mguu hasa baada ya wachezaji wa timu hiyo kuonesha kuchoka kutokana na mikikimikiki kwa baadhi ya misimu na kufanya washindwe kupata matokeo ya kueleweka.

Kwa upande wao The blues wamekuwa na wakati mgumu zaidi haswa wakiwa wanashikilia nafasi ya 10 na kumpa wakati mgumu zaidi mwalimu wa kikosi hicho Ghaham Potter ambaye amefululizwa na matokeo mabaya tangu ajiunge na timu hiyo baada ya Thomas Tuchel kuvunja mkataba na timu hiyo.

Timu zote mbili kwa sasa zina alama 28 katika msimamo wa ligi huku kukiwa na utofauti wa magoli na Liverpool wakiwa na mechi moja mkononi. Odds za Liverpool kushinda au kutoa sare na Chelsea (Double chance) ni 1.25

Leave your comment