Ubashiri Mechi Ya Arsenal Vs Manchester United EPL- Mdundo Alt

[Picha: Arsenal Mania]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Jumapili ya Ligi kuu Uingereza inaendelea kwa Arsenal wakikusanya mitutu yao kwenda katika vita ya kisasi dhidi ya Mashetani wekundu Manchester United katika uwanja wa Emirates.

Licha ya Arsenal kuongoza ligi hiyo ya Uingereza lakini wanaingia katika mchezo huo wakiwa na jeraha dhidi ya United waliowatandika bao 3-1 katika mchezo uliochezwa Old trafford mwezi Septemba ambao pia ndio mchezo pekee Arsenal waliofungwa katika ligi msimu huu.

Manchester United nao pia wamepata pigo katika mechi yao dhidi ya Crystal Place baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Casemiro kupatiwa kadi ya njano, ikiwa ni kadi ya tano ya njano na kumfanya akose mchezo utakaofuata ambao ni mchezo dhidi ya Arsenal.

Kocha wa United Erik Ten Hag amesema kukosa kwa Casemiro katika mchezo huo hakuta leta shida dhidi yao kwani hata katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Arsenal, United walishinda licha ya mchezaji huyo kucheza dakika 10 pekee.

Arsenal kwa sasa wana majeruhi  wachache ukilinganisha na United, majeruhi wa Arsenal ni mshambuliaji Gabriel Jesus, Kiungo Mohamed Elneny pamoja na winga Reiss Nelson.

Majeruhi wa Mwalimu Ten Hag ni pamoja na beki Axel Tuanzebe, Diogo Dalot, pamoja na Don Van de Beek ambaye atakosa mechi za msimu mzima. Habari njema ni kwa Jadon Sancho kurejea mazoezini mara baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda hivyo kuna uwezekano wa mchezaji huyu kujumuisha kikosini siku ya Jumapili.

Mikel Arteta kwa sasa anacho kibarua cha kuthibitisha ya kuwa makosa wakiyoyafanya katika mchezo uliopita yameshafanyiwa marekebisho. Kwa timu zote mbili kupata magoli odds zilizotolewa ni 2.20

Leave your comment