Ufaransa Na Marekebisho ya Kikosi Kuelekea Qatar - Mdundo Alt

[Picha: Reuters FP ]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Zikiwa zimebaki ziku chache macho yote yaweze kugeukia kombe la dunia vikosi mbalimbali vya timu za Taifa vimeendelea kutaja wachezaji wake. Moja ya timu hizo ni pamoja na Ufaransa ambao wao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo la dunia. Jumatano ya wiki hii Ufaransa imetaja kikosi cha wachezaji 26 ambao watashiriki kombe hilo la dunia.

Wakiwa na kocha wao aliowafanikisha kuchukua kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 Dider Deschamps kwa upande wake hakuna mabadiliko aliyoyafanya  kwa walinda mlango kwani Alphonse Areola wa West Ham, Steve Mandanda wa  pamoja na Hugo  Lloris ambaye pia ni Kapteni wa kikosi hicho cha Ufaransa wote wataelekea Qatar.

Marekebisho ya hali ya juu yameanza kujitokeza katika safu ya mabeki wa timu hiyo kwani wachezaji watano katika kikosi hicho ni wapya na hawakuweza kushiriki kombe la dunia lililopita na wachezaji hao ni kama vile William Saliba wa Arsenal, Theo Hernandez kutokea Ac Millan, Ibrahima Konate wa Liverpool,Jules Kounde kutokea Fc Barcelona, pamoja na Dayot Upamecano wa Bayern munich.

Soma pia:  Msanii Vanillah Music Adokeza Jinsi Alivyokutana Na Alikiba

Katika safu ya viungo kocha wa timu hiyo ameibadili safu yote kutoka na sababu za wazi za majeruhi na pengine sababu zisizokuwa za wazi na wachezaji wapya katika safu ya viungo ni pamoja na Youssouf Fofana wa Monaco, Eduardo Camavinga na Aurelien Tchouameni kutokea Real Madrid, Matteo Guendouzi na Jordan Veretout hawa wakitokea Marseille, Adrien Rabiot wa Juventus.

Safu ya mashambulizi  imeanza kwa ingizo jipya la mshindi wa Ballon D’or mwaka huu Karim Benzema kutokea Real Madrid, Christopher Nkunku wa RB Leipzg, pamoja na Kingsley Coman kutokea Bayern Munich.

Baadhi  ya wachezaji watakao kosa kushiriki na timu hiyo ya ufaransa kutokana na majeraha ni pamoja na viungo N’golo Kante ambaye anatarajiwa kurejea mwezi Januari uwanjani huku Paul Pogba wa Juventus akionekana kuendelea vizuri na majeraha yake ya goti.

Leave your comment