Msanii Vanillah Music Adokeza Jinsi Alivyokutana Na Alikiba

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Nyota mpya kwenye muziki wa Bongo Fleva Vanillah Music kwa mara ya kwanza amefunguka ni kwa namna gani aliweza kukutana na Ali Kiba mpaka kusainiwa kwenye lebo yake ya Kings Music.

Siku chache zilizopita Ali Kiba ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya kimuziki nchini Marekani, alimtambulisha Vanillah Music kama msanii mpya kabisa wa Kings Music na kando na utambulisho, Vanillah Music pia ameachia EP yake ya kuitwa Listen To Me ambayo amemshirikisha K2ga.

Akizungumza hivi karibuni, Vanillah Music amedokeza kuwa alikutana na Alikiba kipindi akiwa kwenye maandalizi ya albamu ya Only One King ya kwake Ali Kiba na kwamba mtu aliyrmkutanisha na Ali Kiba alikuwa ni mtayarishaji wa muziki Yogo Beats.

"Nilikuwa nimefanya kazi na Yogo. Yogo yeye alikuwa ameshaona uwezo wangu kama kwa hiyo akanipa nafasi kwa hiyo akanipendekeza. Kwa hiyo nikapata nafasi ya kushiriki kwenye uandaaji wa albamu ya Only One King" alizungumza Vanillah Music.

Aidha Vanillah Music pia alidokeza kwamba katika albamu hiyo ya Only One King, yeye alihusika katika kuandika ngoma ya Utu ambayo ilifanya vizuri sana ndani na nje ya Tanzania.

Kwa sasa ameachia Video ya kwanza kutoka kwenye EP yake ya wimbo "Unanisitiri' na unaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=TcT_rGQsyN4

Leave your comment